Dar es Salaam. Tarehe 13 Disemba 2023: Benki ya CRDB imemkabidhi Rehema Cletus Lupapa, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam gari jipya aina ya Toyota Crown baada ya kuibuka mshindi katika awamu ya tano ya kampeni ya Benki ni Simbanking.
Akieleza namna anavyoitumia huduma za SimBanking, Rehema amesema amekuwa mteja wa Benki ya CRDB kwa miaka mingi na huduma hiyo imekuwa ikimrahisishia kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi na kwa wakati.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi huyo iliyofanyika katika Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama, Dar es salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa, amesema mshindi huyo alipatikana katika droo ya tano ya kampeni hiyo iliyofanyika Disemba 4, 2023 kwenye Makao Makuu ya Wasafi, jijini Dar es salaam.
Rutasingwa, alibainisha kuwa katika kusaidia jitihada za Serikali za kuchochea uchumi wa kidijitali nchini, kampeni ya “Benki Ni SimBanking” imekuwa ikihamasisha wateja kufanya miamala kidijitali kupitia SimBanking na kuachana na matumizi ya pesa taslimu.
Akielezea kampeni hiyo, Rutasingwa alisema “Benki Ni SimBanking” ni kampeni iliyoendeshwa kwa muda wa miezi 10, ambapo kila siku wateja wamekuwa wakijishindia zawadi, huku pia kukiwa na zawadi za mwezi, miezi miwili, na zawadi kubwa ya Toyota Vanguard ambayo itatolewa mwishoni wa kampeni.
“Hadi kufikia sasa tayari tumeshatoa zawadi mbalimbali ikiwamo pesa taslimu, simu janja, na laptop kwa washindi. Hivyo niwasihi wateja na wale wasio wateja waendelee kufanya miamala kupitia SimBanking ili kujijengea mazoea ya kutumia huduma kidigitali,” alisema Rutasingwa huku akiwakaribisha wale ambao sio wateja wa Benki ya CRDB kufungua akaunti ili waunganishwe na SimBanking.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa gari mshindi wa shindano hilo, Rehema Lupapa aliishukuru Benki ya CRDB kwa zawadi hiyo ya gari huku akibainisha siri ya ushindi ni kujenga utamaduni wa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kifedha.
“Ninafurahia sana kufanya miamala kupitia SimBanking iliyoboreshwa, imekuwa rahisi na nafuu sana kutumia. Sasa hivi miamala yangu yote nakamilisha kupitia SimBanking, iwe kufanya malipo kupitia CRDB Lipa Namba, kutuma pesa, kulipia bima, kulipia kodi na kutoa fedha kwa CRDB Wakala/ ATMs na Tawini bila ya kadi,” alibainisha Rehema.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa (wapili kushoto) akikabidhi funguo ya gari jipya aina ya Toyota Crown kwa Rehema Cletus Lupapa (katikati) ambaye ni mshindi katika awamu ya tano ya kampeni ya Benki ni Simbanking, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama, Dar es salaam, Disemba 13, 2023. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili (kushoto), Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd (wapili kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi Huduma za Kidigitali, Mangile Kibanda.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari jipya aina ya Toyota Crown kwa mshindi wa awamu ya tano ya kampeni ya Benki ni Simbanking, iliyofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama, Dar es salaam, Disemba 13, 2023.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari jipya aina ya Toyota Crown kwa mshindi wa awamu ya tano ya kampeni ya Benki ni Simbanking, iliyofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama, Dar es salaam, Disemba 13, 2023.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari jipya aina ya Toyota Crown kwa mshindi wa awamu ya tano ya kampeni ya Benki ni Simbanking, iliyofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama, Dar es salaam, Disemba 13, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments: