Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera akizungumza wakati akifungua mkutano wa madaktari wa kinywa na meno leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Dkt Baraka Nzobo wa pili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Dkt Baraka Nzobo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya Washiriki wa kikao hicho.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimnbali.
Sehemu ya Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka maeneo mbalimbali nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt Wilson Mahera ambaye hayupo pichani wakati alipofungua mkutano wa madaktari wa Kinywa na Meno.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Na Oscar Assenga, TANGA

NAIBU Katibu Mkuu Tamisemi Afya Dkt Wilson Mahera ameviagiza Vyuo vya Afya ambavyo havina kozi ya Shahada ya Udaktari wa Kinywa na Meno kuianzisha ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa watalaamu wengi zaidi hapa nchini.

Dkt Mahera aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati akifungua Mkutano wa Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Kitaifa unaofanyika mkoani hapa ambapo alisema kwamba atafikisha ujumbe huo kwa wakuu wa vyuo hivyo hapa nchini.

Alisema kwamba kufanya hivyo kutawezesha kusaidia upatikanaji wataalamu wengi ambao watasaidia katika utoaji huduma kwa wananchi ambao wanakumbana na changamoto mbalimbali za afya ya kinywa na meno hapa nchini.

“Kupitia mkutano huu niagize vyuo vya Afya nchini ambavyo havina kozi ya Shahada ya Udaktari wa Kinywa na Meno kuanzisha ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa watalaamu hao hapa nchini”Alisema Dkt Mahera.

Katika mwaka 2022 kitaifa kulikuwa na wagonjwa wa kinywa 747,858 waliooza meno 522,777 sawa na asilimia 68.9 ya wagonjwa wote wa kinywa na meno na waliokuwa na matatizo ya fizi ni 78,755.

Alisem kwa takwimu hizo tatizo la kuoza kwa meno bado ni kubwa hapa nchini bado na wana kazi kubwa ya kufanya wagonjwa 156,576 sawa na asilimia 30 walioza meno yalizibwa na wagonjwa 265,249 sawa 49.6 na asilimia walioza meno yaliny’olewa.

“Tatizo la meno yakikubana mtu ukiamka asubuhi yanang’olewa niwatake wataalamu mjikite zaidi kutibu na sio kuyang’oa kwa maana Serikali imewekeza miundombinu yote wezeshi kuhakikisha wananchi wanapatiwa tiba ya meno na sio kungoa jino”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba kuna maeneo ya huduma za kinywa na meno hazipatikani lakini bado wananchi wanatembelea umbali mrefu kufuata huduma hya afya ya kinywa na meno hii sio sawa.

Aidha aliagiza na kuwaelekeza waganga wakuu wa mikoa na Halmashauri kuhakikisha vituo vya afya vya kimkakati na visivyo vya kimkakati kuhakikisha vinaaza kutoa huduma ya matibabu ya kinywa na meno ili kuepusha wananchi kutembelea umbali mrefu.

Hata hivyo aliwataka pia kuhakikisha wanakuwa na vifaa stahiki ikiwemo viti vya kutolea huduma na vifaa vya kisasa zikiwemo mashine za kifanyia uchunguzi wa afya ya kinywa na meno kulingana na miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya.

Awali akizungumza wakati akitoa salamu katika mkutano huo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo alisema kwamba mkoa huo upo salama aliwataka wajumbe kuhakikisha wanakuwa makini vitu ambavyo vitawasilishwa kwenye mkutano huo.

Naye kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Dkt Baraka Nzobo alisema kikao hicho cha Kinywa na meno kwa madaktari kitasaidia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta hiyo.

Alisema tokea wameanza vikao hivyo kila mwaka wameweza kufanya huku akielezea sekta ya kinywa na meno imebebwa sana na ofisi ya Rais Tamisemi kwa sababu Hospitali za wilaya,vituo vya afya,Hospitali Rufaa Kanda na Taifa ni chache.

Alisema kwamba wizara ya afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wakiratibu vikao hivyo na kuna baadhi yao hawatilii mkazo vikao vya maamuzi kwa sababau leo upo nikuombe kuna watu wanaandikiwa barua hawafikia .

“Nikuombe ikikupendeza uwachukulie hatua kwani maendeleo hayawezi kupatikana kama watu wana puuzia vikao vya msingi vya kisekta ambavyo vinaleta mabadiliko katika kutoa huduma bora ya kinywa na meno ofisi hii iliandikia Halmashauri 36 kuleta wataalamu ngazi ya Halmashauri lakini mpaka leo wamefika 17 tunaomba ofisi yao ituulizie kwa wakurugenzi hao 18 kwanini hawajafika mahali hapa wamekaidi”, Alisema .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: