Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga (katikati) akipokea viatu pea 2,800 kutoka katika Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao inayoongozwa na Mwenyekiti wake Steve Mengele (wa kwanza kulia)  pamoja na Katibu wake Msanii Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa ikiwa ni kampeni ya 'Samia Nivishe Viatu' yenye lengo la kuhakikisha wanafunzi wanaotokea katika mazingira magumu wanapata viatu. Makabidhiano hayo yamefanika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Manyara zilizopo Babati.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga (katikati) akionyesha viatu mbele ya wanahabari waliohudhuria makabidhiano hayo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele (wa kwanza kulia) akimuonyesha Mhe. Sendiga ubora wa viatu hivyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele (wa kwanza kulia) akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na uongozo wote kwa ujumla.

Na Cathbert Kajuna - MMG/Kajunason, Manyara.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amepokea Viatu pea 2,800 kutoka katika Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ikiwa ni kampeni ya 'Samia Nivishe Viatu'

Akizungumza katika makabidhiano hayo katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Manyara, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele amesema kampeni ya 'Samia Nivishe Viatu' lengo lake ni kuwapa tabasamu watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

"Kampeni ya 'Samia Nivishe Viatu' inasambaa Tanzania nzima, na sasa imefika Mkoa wa Manyara niwashukuru sana Viongozi wote wa Mkoa na Wilaya mpaka vijiji kwa ushirikiano wao waliotuonyesha kwetu hakika tumefarijika sana," amesema Steve Mengele.

Akitoa shukrani zake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amesema kuwa jambo lililofanywa na taasisi hiyo limeacha alama katika mkoa Manyara hakika watabaki katika mioyoni yao.

"Binafsi sina cha kusema zaidi ya asanteni hili mlilolifanya ni kubwa mno, hivi viatu vitasambaa shule zote za msingi zenye mahitaji maalum, niziombe pia taasisi nyingine kujitoa kuunga mkono maendeleo ya mkoa wetu," amesema Mhe. Sendiga.

Kampeni ya 'Samia Nivishe Viatu' imelenga kuwavika viatu jumla ya watoto 2,000 licha ya mkoa huo kupatiwa pea 2,800 na mpaka sasa jumla ya shule nne zimevalishwa viatu pea 1,000.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: