MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akiwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati akiwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kulia akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Tanga tayari kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Tanga

Na Oscar Assenga, TANGA.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewaonya makada wa chama hicho mkoani Tanga ambao wameanza kujipitisha pitisha kutangaza nia ya kutaka Ubunge na Udiwani waache mara moja maana wakiendelea wanajimaliza wenyewe.

Hemed ambaye pia Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga aliyasema hayo Octoba 8,2023 wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara yake ya kichama kwenye mkoa huo.

Alisema kwenye mkoa huo wapo watu wameanza kujipitisha pitisha wakitangaza nia ya kusaka udiwani na ubunge wakati wakidhana kufanya hivyo ni kosa hivyo niwatake walipofikia wasimame.

“Katika hili niwaonye watu ambao wameanza kujipitisha na kusaka ubunge na udiwani wakati viongozi hao bado wapo hapo walipofika wasimame wakiendelea wataendelea kujimaliza mimi ni mjumbe na wale sitamuoenea aibu mtu wa namna hiyo kwa maana sasa wabunge tunao achene wafanya kazi zao hatutakubali hili”Alisema

Mlezi huyo alisema ukiona mtu ana ndoto ya kuanza kuona anafaa kuwa mbunge na diwani sio pekee yake ana watu huko nyuma wanampa sapoti acheni hizo tabia chama kina utaratibu wake muda ukifika wataangalia nguvu yako .

Aidha alisema kwa sasa kwenye mkoa huo na yeye akiwa mlezi ameona aliseme mapema na kama kuna watu wanawatuma watu hizi hazikubaliki kutokana na taratibu za chama hicho.

“Kama hukufuata nidhamu ya chama haustahili kuwa kiongozi achene jambo hilo sasa tulenge kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tufanye kazi na tuweke nguvu kwenye uchaguzi wa mkuu wa 2025”Alisema

Alisema pia katika mkoa huo hawatakuwa tayari wala kumvumilia mtu ambaye anakwenda kuufanya ushindi wao uwe na tatizo wakati CCM haina tatizo.

Aidha alisema mtu huyo yeye ndio atakuwa tatizo atatupisha yeye kama ni wa serikalini wataangalia utarartibu kwa kumfikishia Taarifa Mwenyekiti wao Taifa Dkt Samia Suluhu kwamba hapa hatuendi vizuri na amekuwa hodari wa kufanya hivyo.

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Makamu huyo wa Pili wa Rais alisema wakati wanaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kauli mbiu ya mkoa huo ni wapo tayari kwa ajili ya uchaguzi huo wa 2024.

Alisema pili ili waende kwenye uchaguzi huo wakiwa vizuri lazima waendelea kuzidisha umoja na mshikamano baina yao wenyewe kwanza hilo anazungumzia kwa viongozi wakishikamana wao wanapokwenda kwa wananchi wanazungumza lugha moja ya ushindi wa CCM.

Alitumia wasaa huo kuwaomba viongozi wa wilaya na mkoa pale penye changamoto wewekane sawa ikiwemo kuondosha tofauti za na wasimame kwenye mstari utakaowaongoza wanachama wao kuelekea kukipigia kura chama hicho kwenye ngazi zote.

Alisema ili kuhakikisha wanashinda kwenye ngazi zote na wakifanya hivyo huo utakuwa ni ujumbe mzuri wa kuelekea 2025 huku akiwaomba wamuomnyeshe Rais Dkt Samia Suluhu na watanzania kwamba Tanga wakiamua wanamaanisha.

Hata hivyo aliwataka waende wakatimize lengo lao huku akiwahaidi kuwa mstari wa mbele kwa sababu hapendi kushindwa.

Makamu huyo wa pili wa Rais aliwataka Mwenyekiti anayehisi kwenye kata yake atashindwa awasamehe mapema kutokana na kwamba hawatakuwa tayari kupoteza chochote kwenye jambo hilo lazima wahakikishe wanashinda.

Kuhusu upinzani.

Alisema kwamba kwa mkoa huo wapinzani watatulia kama wanapakwa hina huku akiwataka kila mtu kwenye wilaya yake huo mkakati wanaimarisha kwenda kushinda kwenye serikali za mitaa.

Makamu huyo wa pili alisema wana malengo ya kwenda kushinda kama kuna jambo halikajaa sawa wawambie kutokana na kwamba chama hicho ni kikubwa na hawawezi kufanya mchezo kuingia kimasihara lazima waingie na wapate matokeo.

Umoja na Mshikamano alisema kwamba suala la umoja kamisaa yupo hapa kaa vizuri na kamisaa wako wa wilaya wote washauriane vema changamoto wamalize huko wakija wanakwenda kwenye utekelezaji na wanakwenda kumaliza shughuli zao na wao wanaendelea kubaki kuwa kidedea.

“Hakikisheni hilo mnalifanyia kazi kwani mkiniona nipo Zanzibar msifikirie ya Tanga siyajui na yanayojiri kwenye vikao najua kila siku nimekuja nikijua Tanga kuna nini niwaombe mshikamano huo ndio utatupelekea ushindi wa CCM. Virus-free.www.avast.com
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: