Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori akizungumza na wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni ya Kutangaza Utalii 'TWENDE TUKACHARU RAU Forest 2023' lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita katika hifadhi ya Msitu wa Rau -Moshi inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mhifadhi daraja la pili msitu wa Rau Zayana Mrisho akisoma risala kwa Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kutangaza Utalii 'TWENDE TUKACHARU RAU Forest 2023' lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita katika hifadhi ya Msitu wa Rau -Moshi inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu akitoa shukrani wa wakazi wa Moshi na viunga vyake waliohudhuria katika uzinduzi katika kampeni ya kutangaza vivutio vilivyopo katika hifadhi ya msitu Rau.
Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori (wa pili toka kushoto) akiwa ameongozana na viongozi wengine wakipata maelezo toka kwa Afisa Uhifadhi wa msitu Rau wakati wakitembelea vivutio vilivyopo katika msitu huo.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG

...KAMPENI YA KUTANGAZA UTALII 'TWENDE TUKACHARU RAU' YAWA KIVUTIO KWA WAKAZI WA MOSHI, KILIMANJARO

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori ametoa rai wa Wananchi kuendelea kutunza hifadhi ya msitu wa Rau na kuacha tabia kutupa taka taka ndani ya hifadhi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kutangaza Utalii 'TWENDE TUKACHARU RAU forest 2023' lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita katika hifadhi ya Msitu wa Rau -Moshi inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Amesema kuwa hifadhi ya Msitu Rau ni mapafu wa mji wa Moshi kwa vile husaidia kufyonza hewa chafu hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha unaendelea kutunzwa na kuacha mara tabia ya baadhi ya watu wanaovamia na kufanya shughuli za kibinadamu.

"Hakikisheni msitu huu unatunzwa, acheni kufanya shughuli za kilimo ndani hifadhi, acheni kuingiza mifungo ndani hifadhi," amesema.
Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori akipitishwa katika mashamba ya mpunga.
Safari ya kutembelea vivutia vya hifadhi ya msitu wa Rau.
Utalii ukiendelea ndani ya hifadhi ya msitu Rau.
Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori akiwa na wageni wengine wakitazama moja ya chemchem za maji zilizo katika msitu huo.
---
Pia ametoa rai kwa TFS na makapuni za watalii kuendelea kuwahamasisha watalii kutembelea vivutuo vilivyopo ndani msitu huo, kwani hifadhi hiyo ipo mita chache kutoka mji wa Moshi na inafikika kirahisi.

Amesema rais Dkt Samia Suluhu amefungua fursa za Utalii kupitia filamu yake 'Royal Tour', hivyo ni vyema kuendelea kuunga mkono juhudi zake ili kuweza kuongeza idadi ya watalii nchini na ndiyo maana Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi wakishirikiana na Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS) Moshi wamezindua Kampeni ya Kutangaza Utalii ikolojia ndani ya Hifadhi ya Misitu wa Rau ili kuongeza idadi ya watalii.

Aliongeza kuwa mpaka sasa hivi hafurahishwi na idadi ndogo ya watalii wanaofika kutembelea msitu huo, lija ya ukaribu uliopo ambapo ni watalii 1,200 tu kwa mwaka hutembelea msitu huo.

Awali akisoma taarifa kwa niaba Mkuu wa hifadhi ya msitu Rau, Mhifadhi daraja la pili msitu wa Rau Zayana Mrisho, amesema  ndani msitu huo kuna chemchem 20 ambazo zinapeleka kuwepo mito mikubwa 3 inayotiririsha maji kipindi chote cha mwaka.

Aidha amesema mito hiyo ni chanzo cha maji inayotumika katika kilimo cha umwagiliaji cha mpunga ambapo hekta takriban 3,000  hutegemea maji kutoka msitu huu.

"Msitu una vivutio vingi ikiwemo mimea pamoja na miti ya asili ambayo haipatikana katika maeneo mengine, ikiwemo Mti wa Mvule ambayo unazaidi ya miaka 200 ni mrefu kuliko yote barani Afrika," amesema.

Aliongeza kuwa utalii mkubwa unaofanyika katika msitu huo ni Utalii wa baiskeli, ibada,  tafiti na masomo, picha, nyuki na kuangalia madhari ya misitu ndege na wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi.

Mazoezi ya viungo nayo yalikuwepo katika ya kuingia msituni.
Waendesha baskeli nao walinyoosha viungo.
Mhifadhi daraja la pili msitu wa Rau Zayana Mrisho akiwakaribisha wageni.
Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu akiwasalimia wageni.
Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori (kushoto) akiwa pamoja na Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu (kulia) wakizindua utalii wa baskeli.
Utalii wa baskeli nao ulifanyika.
Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu amefurahishwa na ubunifu wa kuandaa kampeni ili kutangaza vivutio vilivyopo katika hifadhi ya msitu Rau.

"Nawaomba waandaaji kuendelea kuandaa matamasha mengi zaidi yatakayosaidia wananchi wengi ili waweze kutembelea msitu huo na kujifunza mambo mbali mbali," amesema Meya Kidumu.

Hifadhi ya Misitu Rau ulianzishwa ukiwa na ukubwa  hekari 3526, ambapo kwa sasa ni hekta 584 zimebaki kutokana uvamizi wa Wananchi na kuanzisha shughuli za kilimo.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: