Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman ashiriki katika hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Taifa ya Taifa ya Ubunifu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman ashiriki katika hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Taifa ya Ubunifu.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Mei 16, amemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika Hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Taifa ya Ubunifu pamoja na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka huu wa 2022.

Hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma Tanzania, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini na wa Kimila, Vyama vya Siasa, Wananchi, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Waandishi wa Habari, Wanafunzi, Vikundi vya Burudani, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na Vijana wabunifu.

Pamoja na kuhutubia hafla hiyo, Mheshimiwa Othman aliyeambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, alipata fursa ya kutembelea Mabanda mbali mbali ya Maonyesho ya Ubunifu na pia kupata maelezo ya Wajasiriambali kutoka Ndani na Nje ya Nchi, yakiwemo Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: