Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega ametumia maadhimisho ya Siku ya wanawake,kuwahimiza wanananchi wote nchini Tanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti mwaka huu.

Mariam Ulega ametoa kauli hiyo katika sherehe ya Siku ya Wanawake iliyofanyika Chalinze mkoani Pwani ambapo amesema kwamba mwaka huu Watanzania watakuwa na sensa ya watu na Makazi hivyo ni vema wakashiriki kikamilifu ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wananchi siku ya Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum.

"Sensa ni mchakato maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo amesema Ulega”

Mariam Ulega amewaomba wananchi waendeee kujikinga na korona kwa kunawa minono na kuvaa barakoa pamoja na kuchanja ili kujilinda na kuwalinda wengine wasipate maambukizi ya ugonjwa huoo. Pia amewaomba wananchi waendee kuchapa kazi huku wakichua tahadhari za ugonjwa wa Corona

Hivyo amesema kwenye familia ndoo za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ziwepo, wabebe vipukusi na katika maeneo ya mikusanyiko inashauriwa kuvaa barakoa kwa kuzingatia mwongozo ulitoalewa na Wiza ya Afya.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani, Mariam Ulega(wa pili kushoto)akipokelewa na wananawake wa mkoa huo alipowasiri kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani,Mariam Ulega (katikati) akisalimina na Wanawake wa mkoa wa pwani alipokuwa akiwasili kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Chalinze Mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Wanawake wa mkoa wa Pwani wakishangilia alipokuwa akiwasiri Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani,Mariam Ulega (hayupo Pichani)
Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye kusherehekea siku ya Wanawake Duniani leo Chalinze Mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani, Mariam Ulega (kulia) akiondoka huku akisindikizwa na wanawake wa Mkoa wa Pwani baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: