*Kulaya ashukuru mwitikio wa wadau
Serikali imesema kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya juu ya kuelimisha jamii kuepuka vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu .
Hayo ameyasema na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera Bunge Kazi Ajira Vijana na watu wenye ulemavu Ummy Nderianang wakati wa Kongamano la Wanawake na vijana wenye ulemavu kufikia kuishi kwa huru pamoja na kujua haki zao dhidi ya ukatili katika kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili lilofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kuna haja ya viongozi hao kuendelea kusaidia kwenye eneo hilo kwa maana kuelimisha huku akiitaka jamii hiyo yenye ulemavu kujitokeza hadharani na kujiona kama wanaweza na kamwe asione aibu badala yake ajione kuwa anaweza kufanya kitu chochote bila kujali ulemavu aliokuwa nao.
Amesema kuwa ipo haja ya kushirikiana kwa pamoja na kuwajengea uwezo wanawake hususani wakemavu ili navwenyewe waweze kusisima na kujiamini n kwamba wakijengewa uwezo baadae wanajiamini kufanya kile walichojengwa uwezo.
“Niwaleze kuwa juhudi zote zinazofanywa hususani kwa watu wenye ulemavu lengo ni kupata haki yao ya msingi na wakifanya hivyo watapiga hatua lakini kikubwa nikutokata tamaa” amesema
Naibu Waziri Ummy amewahamasisha walemavu kujitokeza Hospitalini na vituo vya afya kupima afya zao nakwamba katika hilo wasione aibu kwani ni kujali afya zao.
Ameongeza kuwa katika mwaka ujao serikali inakwenda kufanya sensa ya kuhesabiwa ili kujua au kupata takwimu halisi hivyo mchakato utakapofika wajitokeze ili kujua takwimu yao ya kuweza kusaidia mipango yao ya kimaendeleo.
Kwa upande wa ukatili amefafanua kuwa tatizo hilo ni kubwa na kila mmoja anapaswa kuendelea kupinga na kukemea huku akitoa raia kwa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo Barani Afrika WiLDAF kufanya tathimini juu ya ukubwa wa tatizo hilo na ofisi ya Waziri Mkuu iko wazi kupokea yale ambayo wataafikiana.
“Nahimiza kwamba msikate tamaa kwani nyie mnaweza na kama kuna watu wataowakatisha tamaa semeni Ofisi ya Waziri Mkuu.imesema tunaweza kikubwa ni upendo na ushirikiano.”amesisitiza
Pia uzinduzi wa kongamano hilo ulienda sambamba na uzinduzi wa mpango wa mradi wa My Choice my right ambao ni wama ambao unatafasili ya kulinda haki za wanawake na wasichana wenye ulemavu Tanzania.
Kwa upande wake Anna kulaya wakili ,mratibu kitaifa kutoka shirika la wanawake katika sheria na maendeleo Barani Afrika WiLDAF amesema kuna haja na umuhimu wa kuwepo madawati ya kijinsia yanayowalenga watu wenye ulemavu .
” Tunajadili mambo mengi ,Sera ,mifumo kwa ajili ya watu wenye ulemavu kumsingi tunahitaji kujadili mambo mengi na tunashukuru wadau wote kwa kujitoa kwao kwetu na kongamano hili litaibua fursa ya kuangalia mambo mengi yanayohusu walemavu.”amesema
Naye Askofu Dkt Fredrick Shoo ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la kikristo Tanzania (CCT) na Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT akizungumza katika ufunguzi wa kongamano amesema viongozi wa dini wanatambua watu wote bila kuwepo kwa ubaguzi na kuheshimu haki ya kila mtu japo kuna wengine wanafanya ukatili.
Ameongeza kuwa watu ambao wanashiriki katika kufanya vitendo hivyo waache ,wabadilike na watubu kwani maandiko kupitia vitabu vyote yanapinga vitendo hivyo hivyo viongozi wa dini wasimame pamoja na kuungana na wote wanaotetea haki za walemavu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: