NA OSCAR ASSENGA, TANGA
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu –Watu wenye Ulemavu Ummy Ndairemanga amelitaka Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata) kuacha fitina, vigisu na migogoro kwani haina tija na hali hiyo itapelekea kuwachelewesha kufikia malengo yao.
Ummy aliyasema hayo leo wakati wa Kongamano la kuelekea siku ya wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa litafanyika Desemba 3 mwaka huu kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga ambapo alisema kuna watu mabingwa wa kutengeneza makundi kwenye vyama vya wenye ulemavu na kusababisha kushindwa kutekeleza wajibu wao
Alisema lazima wabadilike na kuondokana na dhana ya kuipa nafasi migogoro badala yake wasaidiane ili waweze kutimiza malengo yao kutokana na kwamba hakuna kitu kinachochelewesha kufikia malengo yaoe kama hicho ikiwemo kushirikiana kwa pamoja na kupendana wao wenyewe
“Ndugu zangu pendaneni, saidianeniuongozi ni kuchukuliana kusaidiana acheni chokochoko ukinichokonoa mimi nikadondoka utadondosha na wengine hivyo niwasihi achaneni na mambo hayo badala yake shikaneni”Alisema
Akizungumza mkakati wa serikali kuendelea kuboresha huduma kwa kundi la watu wenye ulemavu ambapo alisema Rais Samia Suluhu amewapa fedha kiasi cha Bilioni 8 kwa ajili ya kujenga vyuo vipya vya ufundi kwa watu wenye ulemavu.
Alisema ujenzi wa vyuo viwili utakwenda sambamba na kukarabati vilivyopo na kwa kuanzia ikiwemo kujenga chuo nyanda za juu kusini ikiwemo Mkoa wa Songwe Halmashauri ya Mbozi.
Aidha alisema chuo kingine kitajengwa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma ambavyo ni vyuo vipya na michoro yake imekwisha ambao walikuwa wanashirikiana na wahandisi na wamemaliza.
“Niwaambie kwamba Mh Rais ameweka pesa tayari ipo hazina wanasubiri michoro ipelekwe na tumepiga hatua na Rais analidhamini sana kundi letu na vyuo vyetu vilivyobakia vyote vikae kwenye mfumo mmoja vipendekeze”Alisema
“Nataka niwaambie hapa Tanga kuna chuo cha Masiwani cha watu wenye ulemavu na Serikali inaboresha vyuo vyote na Rais ametoa fedha milioni 4 kupitia Tamisemi kujenga mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu kwenye shule za Msingi yatajengwa mabweni 50 na hapa Tanga tutajenga mabweni mawili yameeshaanza na yanaendelea vizuri”Alisema
Hata hivyo alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba wanafunzi wenye ulamavu wanatapa shida ya umbali na Rais Samia ameliona hilo na ametoa fedha hizo ili wanafunzi wakae shuleni wasome na kuondokana na changamoto ambazo walikuwa wanakabiliana nazo awali.
“Tunampongeza Rais wetu Samia Suluhu na tuendee kumuunga mkono kwani amedhamiria kuhakikisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: