Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV.
Changamoto ya Uhaba wa Walimu Katika Shule ya Msingi iliopo Kata Kasharu Halmashauri ya Wilaya Bukoba, bado imeendelea kuwa Kizungumkuti, licha ya Shule hiyo kuboreshwa miundo mbinu upya ya Madarasa na Matundu ya Vyoo.
Hayo yamebainika katika hafla ya makabidhiano ya Majengo mapya ya Madarasa Saba pamoja na Matundu Tisa ya Vyoo vya Shule hiyo, yaliyofadhiliwa na Jamhuri ya Watu wa Korea kupitia Shirika lao la GRORY REACH AND HELP FOUNDATION lenye Makao Makuu yake Jijini Arusha, hafla iliyofanyika Shuleni Butainamwa Novemba 08, 2021.
Akisoma Risala Mkuu wa Shule ya Butainamwa Mwl. Venant Byabato kwa Mgeni Rasmi Ndg. Fatina Laay Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba, amebainisha upungufu wa Walimu Katika Shule hiyo ambayo Ina jumla ya Wanafunzi 468 ikiwa na Walimu wanne wa kiume na mmoja wa kike, jumla Walimu Watano suala linapolekea kushuka kwa Taaluma.
Aidha Mwl. Venant mbali na shukrani alizoziwaailisha kwa Wahisani hao, amezitaja changamoto nyingine katika Shule hiyo kuwa Ni Maji, Umeme, Lishe kwa Wanafunzi pamoja na Ofisi ya Walimu. Shule hiyo imejengwa Tena upya na Wafadhili (Wakorea) hao kwa kipindi cha Miezi mitatu ambao waliofika Kijini Butainamwa kwa Shughuli na Huduma za kiroho na kuona hitaji hilo kwa wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: