Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) leo tarehe 28 Novemba, 2021 imeendesha Semina ya kuwajengea uwezo Wakusanyaji Ushuru wa Maegesho wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya matumizi ya mfumo wa Kielektroniki wa Ushuru wa Maegesho (TeRMIS).

Wakusanyaji Ushuru wameelimishwa kuwa na lugha nzuri ya kuwahudumia wateja wa maegesho pale wanapotumia maegesho (Customer Ccare). Pia wameelimishwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuongeza tija na ufanisi katika kutimiza majukumu yao.

Wakusanyaji Ushuru wamehimizwa kuwaelimisha wateja pale wanapotoa huduma ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima.

Mfumo wa maegesho Kidigitali unatarajia kuanza kutumika kuanzia 1 Desemba, 2021 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Singida na Dodoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: