KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati wa wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya filamu nchini.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amewataka wasanii nchini kushiriki kuiendesha tasnia kwa weledi, kujenga umoja na kuiongezea thamani wao wenyewe kwakutoa maoni ya kuboresha kila eneo badala ya kuwa walalamikaji miaka nenda rudi.

Dkt. Abbasi amesema hayo leo Novemba 28, 2021, jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya filamu nchini katika hatua za kujipanga zaidi kuelekea Tamasha la Tuzo za Filamu za mwaka 2021 ambazo Serikali kupitia Bodi ya Filamu imeamua kuzirejesha na zitafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza wakati pia tuzo za muziki na sanaa nyingine nazo zikiwa jikoni.

Amewasisitiza wasanii kuthamini tuzo hizo kwa kuwa zinalenga kuwatangaza ndani na nje ya nchi pamoja na kuwapa hamasa ya kufanya kazi bora zaidi.

“Penye kasoro tuambieni tutaboresha, ukikosa tuzo usinune angalia ulipojikwaa mwakani ufanye vyema zaidi lakini kwa ujumla tuzo hizi ni za nchi wala sio za mtu kwa hiyo tutasimamia haki na weledi,” alisema Dkt. Abbasi kauli ambazo zimeungwa mkono nawadau hao wengi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: