MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP,) umeandaa Warsha kwa viongozi Wanawake na Vijana wa kike kuhusu umuhimu wa uingizwaji na utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika vyama vya siasa 2021.
Warsha hiyo imeandaliwa kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika kutoa maamuzi na uongozi katika miundo ya uongozi. Pia kujadili na kuthamini uchambuzi juu ya masuala ya kijinsia yaliyo ingizwa katika miundo wa vyama vya siasa na kujenga uelewa wa pamoja juu ya Sheria ya vyama vya siasa.
Akiwakilisha mada mratibu wa Taifa mtandao wa Ulingo Dr.nAve Maria Semakafu amewaasa wanawake kujitathmini kuona fursa zilizo mbele yao wajitokeze zaidi kuwania nafasi za uongozi.
Bi Ave Maria amewashauri wanawake kujiwekea utamaduni wa kujitatathimini waonapo changamoto wanazotakiwa kuzifanyia kazi na kuona jinsi gani ya kuzitatua.
Lakini pia amewashauri wanawake viongozi kuwa pamoja kuacha tofauti za kivyama na kuwa na umoja .
Kwa upande wake Mkurugenz Mtendaj wa TGN B. Lilian liundi ametoa takwimu juu ya hali ya uongozi uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi ya uongozi na kueleza kwa bado hawajafika lengo na kueleza kuwa TGNP imekuwa ikitengeneza mikakati ya pamoja ya namna ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa vyama vya kisiasa.
Mratibu wa mtandao wa Ulingo Dr. Ave Maria Semakafu akzungumza katika warsha hiyo na kueleza kuwa wanawake na vjana ni kundi muhimu katika utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika vyama vya sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa jinsa Tanzania (TGN,) Lilian Liundi akizungumza wakati wa warsha hiyo na kueleza kuwa TGNP imekuwa ikitengeneza mikakati ya pamoja ya namna ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa vyama vya kisiasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: