Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla akizungumza na wakaguzi wa dawa wa manispaa za Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa wakaguzi hao hawapo pichani, mafunzo hayo yamefunguliwa katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)leo Novemba 30,2021. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMD), Adam Fimbo na Kulia ni Meneja wa TMDA kanda ya Mashariki (Tanga, Dar es Salaam na Pwani), Adonis Botegeko.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla akizungumza na wakaguzi wa dawa wa manispaa za Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa wakaguzi hao, mafunzo hayo yamefunguliwa katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)leo Novemba 30,2021.

*Asisitiza kufanyika kwa ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kudhibiti wezi na kugundua dawa bandia.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amefungua mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa kwa wakaguzi wa dawa wa manispaa za Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Novemba 30, 2021.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo amewaasa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMD) kupitia mafunzo hayo kupata ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali, hata hivyo ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka, kufanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.

Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeti wa kazi hiyo ambayo inabeba dhamana ya maisha na uhai wa Wananchi.

Ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kubaini wababaishaji na kuwakamata wauzaji wa dawa bandia ili kuokoa maisha ya watu pamoja na kugundua kama wauzaji wa dawa hizo wanasifa na vigezo vinavyohitajika na serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMD), Adam Fimbo amesema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wakaguzi wa dawa wa manispaa za Dar es Salaam ili kujua njia za kutambua dawa na vifaa tiba ambavyo ni bandia pamoja na kujifunza sharia malimbali zitakazo wawezesha kufanya kazi kwa uadilifu.

Fimbo amesema kuwa Zaidi ya wakaguzi wa dawa wa manispaa za Dar es Salaam 33 watapata mafunzo hayo waajifunza kanuni mbalimbali juu ya madhara ya dawa na vifaa tiba bandia pia watapata mbinu za kudhibiti matumizi ya madawa holela na uingizwaji wa vifaa tiba na naihujumu Serikali yakiwamo na maduka bubu ya dawa na maabara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: