Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO'S) mkoani Singida Tumaini Christopher akizungumza jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuyajengea uwezo mashirika hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili Mkuu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS).
Afisa Programu Mwandamizi kutoka FCS Makao Makuu Dodoma Nicholaus Mhozya, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la Iguguno Development Foundation (IDEFO) Vicky Mwaisakila (kushoto) akiandika wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania For Equal Opportunity (TAFEO) Stellah Mwagowa akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la Youth Extended Foundation (YOEFO) Martha Nahson akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Kawawa Munjori, akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mafunzo yakiendelea.
Mkurugenzt wa Utu Wangu Organaition, Fatuma Mgeni akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida Yusufu Msangi akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Singida Development Association (SIDAS) akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Hassan Rasul kutoka Mtinko Education Development Organization, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Adam Mayo kutoka Manyoni Development Foundation (MADEFO) akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) nchini, Dkt.Suleiman Muttani, akizungumza kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali (NGO'S) mkoani Singida yametakiwa kufanya shughuli zao kwa kufuata kanuni na sheria zilizowekwa na Serikali na si vinginevyo.
Hayo yamesemwa jana na Msajili Msaidizi wa mashirika hayo Mkoa wa Singida Tumaini Christopher wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuyajengea uwezo mashirika hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili Mkuu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS).
" Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawajibu wa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria kanuni na sheria za nchi jambo litakalosaidia kuwa tumikia wananchi bila ya bugugha,". alisema.
Mratibu wa mashirika hayo mkoani hapa Patrick Kasango akizungumza kwa niaba ya Serikali alisema Serikali ya mkoa itaendelea kushirikiana na mashirika hayo.
Kasango alitumia nafasi hiyo kuwaomba wawakilishi wa mashirika hayo kwenda kupata Chanjo ya Uviko 19 pamoja na kuihamasisha jamii juu ya umuhimu wakupata chanjo hiyo ambayo Serikali imetumia fedha nyingi kuiagiza kwa kupitia Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
Akitoa mafunzo hayo Mwezeshaji Wakili wa Serikali kutoka ofisi ya msajili, Dennis Bashaka alisema Sheria inayataka mashirika yasiokuwa ya kiserikali kuhakikisha yanafuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao sambamba na taarifa ya mapato na matumizi.
Alisema sheria imeeleza wazi kuwa shirika lisipofanya hivyo kuanzia miaka miwili litafungwa licha ya Serikali kutambua umuhimu wa mashirika hayo kwani kinachohitajika ni kufuatwa kwa taratibu.
Mwezeshaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida Yusufu Msangi aliyaomba mashirika hayo kuzingatia maelekezo yote ya TRA kuhusu ulipaji wa kodi kwa wakati ili kuepuka faini zisizokuwa za lazima.
Afisa Programu Mwandamizi kutoka FCS Makao Makuu Dodoma Nicholaus Mhozya alisema mafunzo hayo yalilenga kuzijengea uwezo taasisi hizo ili kukumbushana masuala muhimu hasa sheria ambazo zinayaongoza mashirika hayo kufanya kazi.
Alisema katika mafunzo hayo walikuwa na mada kuu mbili moja ilijikita kuongelea sheria ya Ngo's ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake na uratibu wa masuala mbalimbali ya kazi za mashirika hayo.
" Mada ya pili ilikuwa ni kuhusu masuala ya ulipaji kodi ambazo zinazihusu asasi za kiraia ambayo iliwasilishwa na mwakilishi kutoka TRA," alisema Mhozya.
Mshiriki wa mafunzo hayo Martha Nahson kutoka Shirika la Youth Standard Foundation (YSF) aliiomba Serikali ifanyie kazi upande wa kodi zinazotolewa na Serikali kwa kuangalia mashirika madogo na makubwa kuwa na sheria zake ili hayo madogo yakifikia hatua ya kukua yahamie huko ili kuyapunguzia mzigo wa ulipaji wa kodi kutokana ya uwezo wao wa fedha za.kujiendesha kuwa mdogo ukilinganisha na hayo makubwa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania For Equal Opportunity (TAFEO) Stellah Mwagowa alisema mafunzo hayo yamewapanua mawazo na kuona jinsi Serikali ilivyojitahidi katika eneo zima la usajili wa taasisi hizo ambao unafanyika kimtandao na kuokoa muda na masuala mazima ya kuendesha miradi na kuzifanya taasisi hizo kuwa endelevu.
"Kuna mambo ambayo bila ya elimu ilikuwa ikionekana kwamba kuziendesha taasisi hizo ni mambo magumu wakati tukijua nchi yetu inazihitaji taasisi hizi kufanya kazi na Serikali katika kuihudumia jamii ukizingatia kuwa zimekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na masuala mazima ya kupambana na umasikini,". alisema Mwagowa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: