Katibu Mkuu wa Umoja Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) , Stella Joel

Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) wametoa salamu za rambi rambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021katika Hospitali ya Mzela jijini Dar es Salaam.

Salamu hizo za rambi rambi pia wamezitoa kwa Waziri Mkuu, viongozi mbalimbali, mjane wa marehemu Janeth Magufuli ,Rais wa Zanzibar na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema kifo cha Rais Magufuli wamekipokea kwa mshituko mkubwa na kuwa watamkumbuka milele daima.

"Tunamshukuruaa Mungu kwa ajili ya maisha ya Rais Magufuli ambaye katika uongozi wake aliinua Tasinia ya Muziki kwa kuwasaidia wasanii kwa kutatua changamoto zao mbalimbali" alisema Joel.

Alisema Rais Magufuli alifanikiwa kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kwa kuwa jali wanamuziki hao upande wa kiafya kwa Kuwapatia Bima ya Afya ya NHIF kwa gharama nafuu kwa ajili ya vipimo na matibabu katika Hospitali za Serikali na za Binafsi.

Joel alisema alikuwa katika maandalizi ya kufanya maboresho mengi ili wanamuziki waweze Kufaidika na kazi zao.

" Hakika tutamkumbuka Magufuli kwa mema mengi aliyoyafanya enzi za uhai wake kama Rais wa Tanzania"alisema Joel.

Stella alisema kwa niaba ya TAMUFO ana mpongeza Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa wana amini atayaendeleza yale yote ambayo Hayati Rais Magufuli aliyokuwa ameyaanzisha ambapo wanatambua kwamba kazi hiyo walishirikiana Pamoja.

" Tunakuombea Rais Mama Samia Mungu awe pamoja naye katika kutekeleza yale yote na sisi wanamuziki tumepokea kwa furaha kwa kuapishwa na kuwa Rais wa kwanza Mwanamke katika nchi yetu." alisema Joel.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: