Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji a Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) pamoja na watendaji wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali moani Mbeya,walipoanza ziara yao ya kufuatilia utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali za wanyonge kwa kukutana na wadau walionufaika na urasimishaji huo Januari 26, 2021. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Daniel Ole Njoolay ikiwa katika kikao cha kutambulishana kwenye ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo. 
Wakitoka kwa Mkurugenzi kuelekea kwa Mkuu wa wilaya.
Timu ikielekea Ofisi za Wilaya ya Mbarali kukutana na Mkuu wa Wilaya pamoja na wadau wanufaika wa Mkurabita.
Timu ikiwasili Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.
Wakiwa kwenye kikao cha utambulisho ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune (kulia). Kushoto ni ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Balozi mstaafu Njoolay.
Balozi mstaafu Njoolay, akizungumza wakati wa kikao na wadau walionufaika kwa kujengewa uwezo na Mkurabita wilayani Mbarali. ambapo zaidi ya wananchi 988 wamekopa benki zaidi ya sh. bilioni 19 kwa kutumia Hati za Hakimiliki za Kimila kama dhamana.
Mratibu wa Mkurabita, CPA Dkt. Seraphia Mgembe akielezea jinsi alivyofurahishwa na wadau walivyochangamkia fursa ya kutumia kukopa benki kwa kutumia Hati za Hakimiliki wilayani Mbarali.
Ofisa Mikopo kutoka Benki ya NMB, akielezea walivyofanikisha wanufaika wa Mkurabita kupata mikopo kwenye benki hiyo ambapo hadi sasa 155 wameshakopa zaidi ya sh. bilioni 7.
Afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya ya Mbarali, Geofrey Mwaijobele akisoma taarifa ya wilaya kuhusu mafanikio ya urasimishaji wa rasilimali za wanyonge baada ya kujengewa uwezo na Mkurabita.
Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Gabriel Mfune akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Mkurabita na wadau walionufaika na mikopo kutumia hati za hakimiliki za kimila.
Baadhi ya watendaji wa Mkurabita
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mfune akiwa na wajumbe na baadhi ya watendaji wa Mkurabita
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mfune (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mkurabita. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi, Balozi mstaafu Njoolay na kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi Immaculata Senje na Mratibu wa Mkurabita, Dkt. Seraphia Mgembe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: