Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume akionyesha karatasi ya kupigia kura kwa wajumbe wa kamati wa chama hicho
Mshindi wa kura za maoni Joseph Kamonga akiwapungia mikono kuwasalimia wajumbe wa kamati kuu wilayani Ludewa.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura wakisimamiwa na katibu wa UWT Ludewa Flora Kapalia(kushoto)
Baadhi ya wagombea wa kura zamaoni kutoka kushoto ni Dk. primus Nkwera, Dk. Evaristo Mtitu na Dk. Neema Mturo
Mshindi wa kura za maoni Joseph Kamonga akinadi sera zake kwa wajumbe wa kamati kuu CCM wilayani Ludewa.
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume kushoto, katibu wa UWT Ludewa, pamoja na wajumbe wengine wakikagua karatasi zilizopigwa.

Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Wagombea wa kura za maoni jimbo la Ludewa mkoani njombe wameupongeza uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusimamia vizuri zoezi la upigaji kura na kuhakikisha kuwa umekuwa uchaguzi wa uhuru na haki.

Akizungumza mmoja wa wagombea hao kwa niaba ya wagombea wenzake kaptain Jacob Mpangala alisema kuwa utaratibu uliowekwa kwa uchaguzi huu ni wa wazi ukilinganisha na chaguzi zilizopita kitu ambacho kinasaidia kuepusha migogoro kwa wagombea kuhisi kufanyiwa hujuma.

Aliongeza kuwa wote kwa pamoja wanakubaliana na matokeo yaliyopo na watayavunja makundi yao na kumuunga mkono mgombea aliyepita.

Aidha katika uchaguzi huo Joseph Kamonga aliibuka mshindi kwa kupata kura 320 katika kura zilizopigwa na wajumbe 718 akifuatiwa na Dk. Philipo Filikunjombe aliyepata kura 191.

Wagombea wengine ni Dk. Susan Kolimba kura 76,Deo Ngalawa kura 62, Dk. Saimoni Ngatunga kura 14, Kamishna Crodwick Mtweve kura 12, Dk. Primus Nkwera kura 8, DK. Evaristo Mtitu kura 7,Dk. Luka Mkonongwa kura 5, Mwl. Fikiri Mgina kura 4, Dk. Beda Mwang’onde kura 3, Dk. Neema Mturo kura 3,James Mkinga kura 2, Deogratius Nchimbi kura 2, Augustino Ngairo kura 2, Jacob Mpangala kura 2, Augustino Mwinuka kura 1, Andru Kuyeyana kura 1, Eng. Alfales Chengula kura kura 1, Baraka Lucas kura 1, Gerecius Lugome kura 0, Mwl. Herman Yanga kura 0, Mwl. Renatius Njelekela kura 0, Barnaba Mhagama kura 0.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: