Naomba nisisitize kuwa Siku ya jana tareh 16 /12/2018 Mimi Nasibu Abdul Juma Issaack, na nilokuwa Nasafiri nao Tokea Mwanza Sikuchelewa ndege Kabisa...Nilifika Muda Sawia kama Usafiri wa ndege za ndani unavyotaka, na kulidhihirisha hilo.. nikiwa niko pale kuna hata Abiria wengine waliingia nusu saa baadae, tena nikiwepo nimesimama palepale... na mmoja ya watu waloingia nikiwepo nimesimama ni @Harmonize_tz ... kilichotokea ni kuwa Mmoja ya watu wenye dhamana pale, siti zetu aliziuza kwa abiria wa fastjet... kwa abiria watalii wazungu, na walichokuwa hawajajua pia waliwauzia na baadhi ya Watu ambao ni wafanyakazi wetu wa Wasafi Media...
Na Kuthibitisha tena kuwa hatukuchelewa, alikuja tena mtu wa Air Tanzania na kutuambia kuwa siti zimebaki mbili... Hivyo tuchague watu wawili tu wasafiri... kama kweli tulichelewa, sasa hao wawili, sasa wangewezaje ingia??? tukasema hatuwezi safiri wawili lazima tuwe wote kama tulivyokata... hivyo ni dhahiri kuwa hatukuchelewa... ila kutokana na Ndege nyingi za kuja mwanza zilicancel Trip zao, ikiwepo Fastjet hivyo Tickets zikawa ni Dili sana na ndio yote kutokea...
USHAURI tu kwa ndugu zetu waliopewa dhamana ya kuliendesha shirika letu la Air Tanzania... tutambue kuwa Mhe Rais, pamoja na Serikali nzima kwa ujumla imepambana Usiku na Mchana, imeamua kujinyima na kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha watanzania nasi tunakuwa na ndege zetu, kwa kuamini kuwa licha tu ya kuingiza kipato, lakini uwepo wa Air Tanzania ni heshima na fahari kwenye nchi Yetu...
Hivyo tunaomba mzisimamie vizuri... na nikiwa kama Mtanzania Mzalendo mwenye akili timamu, siwezi tu kukurupuka kusema jambo kwani ni jukumu langu kuhakikisha nalilinda shirika hili, nalitangaza na kuwasifia wanapopatia lakini pia ni jukumu langu kuwaambia mnapokosea ili mfanye marekebisho na Air Tanzania kuwa shirika bora duniani na kuipa sifa nchi yetu...
Nikiwa kama Mtanzania mwenye uchungu siwezi kuona mtu aliopewa dhamana ya kuzisimamia ndege hizo anafanya vitu tofauti halafu eti nikakaa kimya... Ni sawa na kumvunja moyo Mhe Raisi na Serikali nzima kwa juhudi zake hizi... hivyo Mliopewa dhamana tunaomba muwe makini, na kusimamia vyema ili tusitie doa kwenye ndege zetu...
Toa Maoni Yako:
0 comments: