Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na watumishi wa Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida leo baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula, akiwa ndani ya gari la polisi muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), alipokuwa ziara katika Wilaya hiyo, lengo ikiwa ni kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara za wizara, mkoani Singida. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula(kushoto), akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kushuhudia gari la polisi (pichani), lililoletwa kwa ajili ya shughuli za kudhibiti uhalifu, Naibu Waziri yupo mkoani Singida lengo ikiwa ni kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara za wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Askari Polisi wa Kituo cha Nduguti kilichopo Wilayani ya Mkalama, mkoani Singida leo baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Polisi wilayani Mkalama, John Ntalima, mkoani Singida Leo, ikiwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Toa Maoni Yako:
0 comments: