Na Mwandishi Wetu.

Wazee wameshauriwa kutokaa kimya na badala yake kuchukua hatua madhutubi wanapoona uongozi unayumba katika kusimamia uhai na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo yao.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Mwanasheria wa CCM, Wakili wa Kujitegemea Mwesigwa Zaidi wakati akizungumza kwenye kikao cha Wazee, katika Tawi la CCM la Muloganzira lililopo Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amewasihi Wazee hao kuhakikisha wanakemea tabia inayoanza kuota mizizi ndani ya CCM ya kumtegemea mtu badala ya Chama, tabia ambayo alisema ni hatari sana kwa uhai wa CCM kwa kuwa wengi wanaopenda kusujudiwa ndani ya Chama ni watoa rushwa na mafisadi.

Wakili Mwesigwa mewaomba wazee kuwashawishi watoto wao wenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi mbalimbali ndan ya CCM kujitokeza na wasiwe na hofu kwa sababu uongozi wa juu wa CCM uko imara kuhakikisha hakuna mtoa rushwa wala fisadi yeyote atakayenunua uongozi ndani ya CCM.

Amewataka kuziunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akissisitiza kuwa ndiyo njia salama ya mafanikio kwa watoto wao waliowasomesha katika mazingira magumu.

"Ndani ya CCM hakuna mtu maarufu wala nguvu zaidi ya CCM isipokuwa CCM yenyewe. Waliondoka wengi lakini CCM imezidi kuwa imara zaidi ilivyokuwa siku za nyuma", alisema Mwesigwa.

Akizungumzia kuhusu rushwa na ukiukwaji wa maadili ndani ya CCM Wakili Mwesigwa amesema CCM ina mkono mrefu na uchafu huo unashughulikiwa ipasavyo na na hivyo kuwasihi wazee hao wazidi kuwa na imani na CCM, Rais Maguli na serikali kwa jumla.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwa lengo la wazee kutadhmini uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika tawi hilo la Mulonganzira, Wakili Mwesigwa alihudhuria kwa kwaliko wa wazee hao kuwa mgen rasmi na mtoa mada kuhusu itikadi ya Chama.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: