Mkutano wa mwaka wa 45 wa wanahisa wa kampuni ya TBL Group umefanyika jijini Dar es Salaam ambapo licha ya changamoto mbalimbali za kibiashara,kampuni imeweza kuendelea kufanya vizuri na inaendelea kufanikisha mikakati ya kuifanya biashara yake kuimarika zaidi,kuwa endelevu na kunufaisha jamii.
Kutokana na mafanikio hayo kampuni imetoa gawio la hisa kiasi cha shilingi 770/-kwa kila hisa kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa kampuni uliomalizika ikiwa ni ongezeko la asilimia 28% kulinganisha na gawio la shilingi 600/-lililotolewa katika mwaka wa 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin, ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Masoko cha kampuni mama ya ABInBev kanda ya Afrika Mashariki alisema mafanikio makubwa ya kampuni yametokana na mkakati wa kuimarisha masoko hususani kwa kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa ambazo wananchi wengi wanamudu kuzitumia.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group , Roberto Jarrin (wa pili kushoto) akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka 2018 wa Wanahisa wa Tanzania Breweries Ltd (TBL Group) wa kujadili maswala mbalimbali ya Kampuni uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Cetre Dar es Salaam, wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa TBL Bruno Zambrano, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi , Cleopa Msuya, Katibu wa Kampuni Huruma Ntahena na Mjumbe wa Bodi hiyo Leonard Mususa.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanzania Breweries Ltd (TBL GROUP) Cleopa Msuya wa (katikati) akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka 2018 wa Wanahisa wa Kampuni hiyo .
Baadhi ya wanahisa waliohudhuria mkutano wakitoa michango yao ya mawazo
Baadji ya wanahisa wa TBL waliohudhuria mkutano huo katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa kampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments: