Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), inawatangazia wateja wake wote wa jiji la Dar es salaam, pamoja na Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Majisafi kwa baadhi ya maeneo kwa wastani wa Saa 24, kuanzia saa 12:00 asubuhi siku ya Jumatatu tarehe 27/08/2018 hadi saa 12:00 asubuhi, siku ya Jumanne tarehe 28/07/2018.

Sababu za ukosefu wa Majisafi:

Ni kufanya matengenezo ya mabomba makubwa ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini katika mto Mpiji Bagamoyo

Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na:

Kerege ccm, Kerege kiweti, Kerege amani, Kerege matumbi, Kerege manofu, Mapinga, Mingoi, Kiharaka na Kiembeni

Dawasco inawaomba radhi wananchi wa maeneo husika kwa usumbufu utakaojitokeza

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE).

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: