Meneja wa Masoko na Udhamini wa TBL Group George Kavishe akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusindikiza washindi wanaokwenda Urusi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro,katika uwanja wa ndege wa JK.Nyerere.
Ujumbe wa washindi wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda Urusi.
Ujumbe wa baadhi y washindi ukiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar e Salaam,tayari kwa safari ya kwenda Urusi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro na Kombe la Dunia.
*Wengine waendelea kujishindia mamilioni ya fedha taslimu
Bia rasmi ya Tanzania katika msimu huu wa kombe la dunia ya Kilimanjaro Lager,ya kampuni ya TBL,imefanikisha ndoto za watanzania 10,ambao wamejishindia safari ya kugharamiwa safari ya kwenda nchini Urusi kuona baadhi ya mechi za michuano hiyo mikubwa ya soka ya FIFA Duniani kupitia promosheni yake ya Kombe la Dunia iliyozinduliwa rasmi nchini Mei 12,2018.
Washindi hao 10 wameondoka jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates kuelekea Rusia,wamepatikana kwa kushiriki katika promosheni hiyo ambapo zilifanyika droo mbalimbali chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (Tanzania Gaming Board).
Akiongea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,wakati wa kuwaaga washindi hao,Meneja Masoko na Udhamini wa TBL,George Kavishe,alisema kuwa anayo furaha kuona bia ya Kilimanjaro ya TBL inafanikisha safari ya baadhi ya watanzania kuona mashindano ya Kombe la Dunia mubashara kutoka viwanjani nchini Urusi.
Kavishe alisema kuwa washindi hao wataweza kuangalia mechi mbalimbali zitakazochezwa katika kipindi watakachokuwa nchini humo kabla ya kurejea nyumbani,Juni 30,2014
“Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018 na promosheni inaendelea pia kwa wateja kujishindia fedha taslimu shilingi milioni moja kwa wiki kwa wiki kumi,na muda wa maongezi wa simu wa shilingi 2,500/- ,kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma namba iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki Kumi.
Akiongea kwa niaba ya washindi wenzake,Charles John kutoka mkoani Geita,alisema kuwa wanayo furaha kuona safari yao inatimia ya kwenda kushuhudia mechi za kombe la dunia mubashara viwanjani nchini Urusi na alishukuru bia ya Kilimanjaro kupitia promosheni yake kwa kufanikisha safari hiyo.
Alisema kuwa anaamini kupitia safari hiyo mbali na kupata burudani ya soko pia wataitangaza Tanzania bila kusahau kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawajakutana nayo kabla “Safari hii inaleta furaha na kuleta kumbukumbu ambazo si rahisi kuzisahau maishani”.Alisema John Kwa furaha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: