Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari mkazi wa Geita Pasquina Ignas, baada ya kuibuka mshindi wa matumizi ya Mpesa wakati wa hafla ya kuadhimisha mika 10 ya Mpesa,Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Mworia Rosalynn(kushoto) akishuhudia.
Mshindi wa kutumia huduma za Mpesa mkazi wa Geita Pasquina Ignas, akionyesha namba ya gari baada ya kukabidhiwa kwenye hafla ya kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa Mpesa, kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Mworia Rosalynn na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) wakishuhudia.
Mshindi wa kutumia huduma za Mpesa mkazi wa Geita Pasquina Ignas, akipanda kwenye gari yake baada ya kukabidhiwa jijini Mwanza kwenye hafla ya miaka 10 ya Mpesa.
Wasanii wa kikundi cha Bujora wa mkoani Mwanza wakitumbuiza.
Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali jijini Mwanza, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Mpesa.
Wasanii wa kikundi cha The Happy center, wakitumbuiza kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza ya kuadhimisha miaka 10 ya Mpesa.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella (aliyevaa kofia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia, wakati wa hafla ya miaka 10 ya Mpesa iliyofanyika jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: