Mratibu wa vituo Binafsi Manispaa Ilala, Dkt Wile Sangu akifungia Maabara Bubu na vituo bubu Kijiwe Samri Kiwalani kwa kosa la kutoa huduma bila kibali, katika oparesheni endelevu ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam jana (PICHA NA HERI SHAABAN).
Na Heri Shaaban.
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imezifungia maabara bubu na maduka ya dawa yasio na sifa ambayo yanatoa huduma kinyume cha sheria. Oparesheni ya kuzifungia maabara hizo pamoja na maduka ya dawa imeanza Dar es Salaam jana katika Jimbo la Segerea, Ukonga na Ilala.
Akizungumza jana kuhusu operesheni hiyo Mratibu wa Vituo Binafsi Manispaa ya Ilala Dk.Wille Sangu amesema maduka ya dawa ambayo wanayafungia ni ambayo wahudumu wake hawana sifa za kuendesha huduma hiyo na wengine wanatoa huduma za kuwachoma sindano wateja tofauti na kibali chao.
"Ofisi ya Mganga Mkuu Ilala imeweka utaratibu wake kila mwaka kufanya ziara ya ukaguzi wa kuzikagua maabara bubu ambazo hazina vibali na duka za dawa mara baaada kuwakamata kuwataka wafuate taratibu za usajili ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala,"amesema Dk.Sangu.Amefafanua katika oparesheni hiyo pia wameyanga maduka ya dawa waliyoyakuta watoa huduma hawana sifa na maduka mengine yakijiusisha na upimaji VVV, utoaji mimba na uchomaji sindano.
Amewataka watoa huduma wote ambao wamekamatwa kwenda ofisi za Manispaa ya Ilala kwa ajili ya taratibu Dk.Sangu amewataka wananchi watumie vituo vya tiba kwa ajili ya matibabu ya maabara kwa ajili ya vipimo na maduka ya dawa kwa ajili ya kununua dawa."Ukikuta duka la dawa linatoa tiba au huduma za maabara ni hatari kwa afya yako na toa taarifa kwetu,"amesisitiza.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dk. Emily Lihawa amewataka wamiliki wa vituo vya kutolea huduma katika wilaya hiyo, wafuate miongozo yote ya hutoaji huduma ya afya. Pia amewataka wamiliki watoe huduma kulingana na vibali vyao wasikiuke kanuni,kikubwa wafuate miongozo ya kukinga na kuthibiti maambukizi wakati wa utoaji huduma za afya. Katika ziara hiyo ilifungia maabara bubu na Zahanati Kiwalani, Tabata, Kivule na Minazi Mirefu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: