Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Maofisa wa kitengo cha habari cha mradi wa mabasi ya endayo haraka (UDART) mara baad ay kutembelea mradi wa huo na kujionea mapungufu yaliyojitokeza na kusisitiza kuwa kila mbia ahakikishe changamoto zilizopo zinamalizika haraka.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akimsikiliza mmoja wa Watendaji wa kitengo cha habari katika mradi wa UDART , Joel Beda wakati alipofika katika makao makuu ya ofisi hizo Jangwani Dar es Salaam.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiwa ndani ya moja ya mabasi yaendayo haraka mara baada ya kuamua kupanda kuchanganyika na wananchi.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja ya watendaji wa UDART Katika kituo cha Kimara ambapo alikwenda kujionea msongamano wa abiria katika eneo hilo.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akipita katika eneo la kupita abira kuingia kituoni mara baada ya kukata tiketi na kujinea changamoto iliyopo katika mfumo wa ukataji tiketi katika kituo hicho kutokana kuwepokwa msonagamano mkubwa.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiwa katika foleni ya ukataji wa tiketi kwa mabasi yaendayo haraka UDART.
Mmoja ya wakazi wa Kimara akitoa maoni yake kwa Waandishi wa Habari akiomba mradi huo uboreshwe zaidi.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiwapungia mikono wakazi wa kimara wakati akiwa anondoka katika eneo hilo.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiagana na Mmoja wa Watendaji wa UDART Sabri Mabrouk mara baada ya kumaliza kutembela mradi huo.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ameiomba serikali ifute kodi kwa mabasi ya mwendokasi 70 yanayotarajiwa kuingia ili yaingie nchini na kurahisisha usafiri katika mradi huo ambao kwa sasa unasua kutokana na kuzidiwa na wingi wa abiria.
Kubenea ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kituo cha Mwendokasi cha Kimara Mwisho ili kuangalia changamoto zilizopo katika mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART).
Amesema ameambiwa changamoto kubwa iliyopo ni magari hayo kuwa machache ukilinganisha na wingi wa abiria ambao wanautumia usafiri huo.
"Niiombe serikali ifute kodi ili haya magari yaweze kuingia au itoe muda fulani wa kulipa kodi angalau miezi sita hivi huku usafiri ukiendelea kutumika.
"Inawezekana magari haya yanashindwa kuingia kwasababu muhusika amekosa kodi ya kulipa ndo maana yanachelewa kuingia," amesema Kubenea.
Kubenea amesema wao kama wabunge wa Dar es Salaam pamoja na madiwani watahakikisha wanaulinda mradi huo ili udumu kwaajili ya kizazi kijacho.
"Dar es Salaam ni kitovu cha Nchi, hivyo usafiri unapokuwa wa shida unaathiri mambo mengine. Sisi kama wabunge tunaowajibu wa kuulinda mradi huu na tutahakikisha tunaulinda,".
Amesema atazungumza na wabunge pamoja na Waziri wa Tamisemi kujua wanafanyaje kuulinda mradi huo pamoja na kupata eneo kwa ajili ya karakana.
Aidha Kubenea amesema mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG) ni mzuri na utasaidia katika kuokoa wanaokwepa kodi pamoja na upotevu wa fedha.
Naye Mkuu wa Idara ya Mawasiliano (UDART), Deus Bugaywa amesema ni kweli wanakabiliwa na changamoto kutokana na abiria kuwa wengi kuliko mabasi yaliyopo.
Aidha amesema mbali na changamoto hiyo pia mafuriko yaliyotokea hivi karibuni yamefanya kampuni hiyo kutikisika hivyo wanaomba kama kuna uwezekano wapate eneo lingine kwaajili ya karakana.
"Wakati tunaanza tulianza vizuri....muundo wa mradi ulikuwa yaingie 305 lakini yakaingizwa 140 kwaajili ya majaribio ambapo mwanzo tulikuwa tunahudumia abiria 50,000 kwa siku.
"Lakini sasa hivi abiria wameongezeka tunahudumia abiria kati ya 150,000 hadi 200,000 kwa siku, hivyo utaona abiria wameongezeka lakini mabasi machache,"amesema Bugaywa.
Hata hivyo amesema muda si mrefu mabasi 70 yataingia ambapo wanaimani yatasaidia kuondoa changamoto hiyo.
"Changamoto ya abiria tunaimani yakija mabasi haya itapungua...lakini tunaomba tupate eneo la karakana ambapo mabasi yatakuwa yanahudumiwa kama kawaida tofauti na eneo hili ambalo tunapata changamoto wakati wa mvua," amesema.
Akizungumzia tatizo la tiketi kutafanya kazi kwenye mageti ya kuscan, Bugaywa amesema hiyo inatokana na mabadiliko ya mfumo mpya wa malipo ambapo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Juni.
"Mageti ya kuscan tiketi hayafanyi kazi kwasasa mpaka pale mfumo utakapokamilika na hiyo itakuwa ni mwishoni mwa Juni kwa mujibu wa wataalam," amesema Bugaywa
Toa Maoni Yako:
0 comments: