Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameonya watumishi wa kanisa hilo wanaotumia muda mwingi kupiga picha wakati wa ibada, na kuwataka kujishughulisha kwa Mungu zaidi.

"Mchungaji husema 'inueni mioyo yenu'. Wala hasemi, 'inueni simu zenu mpige picha,'" Francis amewaambia makumi kwa maelfu ya watu waliokusanyika katika kongamano la kila wiki katika Medani ya Mtakatifu Petro, akirejea sala ya komunio katika Makutano ya Romani Katoliki.

Katika mahubiri yake, amesema utumizi wa simu katika Ibada ni "kitu kibaya mno," akaongeza:

"Inanihuzunisha sana ninaposherehekea Ibada hapa upenuni ama kwenye basilika na kuona simu nyingi sana zikiwa juu. Sio tu kwa waamini, lakini pia kwa wachungaji na maaskofu!"

"Ibada sio onesho...hivyo kumbukeni, hakuna kutumia simu!" Papa amesema na kuzua vicheko na makofi kutoka kwenye umati uliohudhuria.

Papa Francis kiongozi wa waumini bilioni 1.2 wa Romani Katoliki, mara nyingi amekuwa akiwaasa waamini kujikita kwenye masuala ya kiroho zaidi huku wachungaji na maaskofu wakitakiwa kuwa wanyenyekevu.

Muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa mwaka 2013, alisema anaumia sana kuona wachungaji wakiendesha magari ya kifahari na kukimbizana na mitindo mipya ya simu janja (smartphone).

Papa anaendeshwa kwenye gari la kawaida Ford Focus lenye rangi ya bluu na hajawahi kuonekana na simu ya mkononi tangu kuchaguliwa kwake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: