Maelekezo Muhimu.
- Wahitimu wa kidato cha sita mwaka
2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo,Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita,Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbijiwamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi. - Wahitimu hawa waliochaguliwa
wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoakama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wakuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014. - Zoezi la usajili litaanza
shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanziatarehe 16/12/2014 hatapokelewa. - Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda
wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shuleya Polisi Tanzania mjini Moshi. - Vijana hawa watalazimika kufika
shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo: - Vyeti vyao vyote vya masomo (original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth
certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. - Mashuka mawili rangi ya Bluu
Bahari (light blue) - Chandarua chenye upana futi
tatu - Nguo za michezo(Track suit
nyeusi,Tshirt blue na Raba) - Pasi ya Mkaa Ndoo moja
- Pesa za kulipia bima ya afya
kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=). - Pesa kidogo ya kujikimu.
- Kwa mujibu wa kanuni za shule
ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikanana simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanyamawasiliano. - Angalia orodha kwenye tovuti ya
www.policeforce.go.tz au fikaOfisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara yamahakama kuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: