Jana 21.10.2014 mapema asubuhi Mratibu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliongea na waandishi wa habari juu ya ufafanuzi wa kashfa mbali mbali zilizomzonga Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu na moja ya jambo ambalo limewakera watu wengi si suala la umri la miss huyu ambapo kumeonekana kujikanganya kwa kushindwa kujibu maswali ya waandishi wa habari.
Moja ya swali kubwa lililokuwa likimzonga ni kuhusu kuzaliwa kwake ambapo alisema kuwa yeye amezaliwa 31.5.1991 wakati vielelezo vyake mbali mbali alivyokuwa akitumia mchini Marekani ikiwemo pasi ya kusafiria (passport) na leseni ya udereva ilikuwa ikionyesha amezaliwa 31.5.1989.
Alipobanwa na waandishi aeleze ni kwanini alikuwa na nyaraka ambazo zilikuwa zinapingana miaka alisema hayo ni maisha yake binafsi tofauti kikubwa yeye alipochukuliwa kugombea miss Tanzania hawakuwa wanahitaji vitu kama pasi ya kusafiria (passport) na leseni ya udereva(driving licence) wao walihitaji cheti cha kuzaliwa.
Kwa uchunguzi uliofanywa na Kajunason Blog unaonyesha kuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu alishiriki mashindano ya ngazi ya Kitongoji bila ya kuwa na vyeti cha kuzaliwa maana mchakato wa kumsaka Miss Chang'ombe mwaka 2014 ulianza Juni 16, 2014 ambapo Mwandaaji wa Mashindano hayo Tom Chilala aliwataambulisha warembo wapatao 17 na Sitti Mtemvu alinyakuwa taji hilo akifuatiwa na Pauline Elisante na wa tatu Darena David.
Picha inamuonyesha Sitti Mtemvu baada ya kunyakua Taji la Chang'ombe 2014.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Sitti alisema baada ya ushindi huo sasa macho yake yote yapo katika kutwaa taji la Miss Temeke, ambalo alidai ana uhakika wa kulipata.
Ukitaka kusoma zaidi hapa;-
Heka heka zilienda Miss Temeke ambapo warembo walitangazwa mbele ya mkutano na waandishi wa habari Juni 26 ambapo shindano lilifanyika katika ukumbi wa TCC Chang'ombe Agosti 23, 2014 na kupatikana mshindi ambaye alikuwa ni Sitti Mtemvu.
Mshindi wa taji la Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu akipungia mkono mara tu baada ya kutangazwa rasmi kuwa ndie aliestahili kupata taji hilo katika shindano lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mshindi wa pili,Salama Saleh na kulia ni Mshindi wa tatu, Neema Mollely.
Zaidi unaweza kusoma link: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/washiriki-wa-miss-temeke-2014-hawa-hapa
Baada ya mashindano kumalizika washindi wote waliochaguliwa waliingia kambini ili kujiandaa na mashindano ya Miss Tanzania 2014 ambapo warembo kutoka pande zote za Tanzania, wapatao 30 waliingia Kambini mnano Septemba 13, 2014 katika Hoteli ya JB Belmont iliyopo jijini Dar es Salaam.
Warembo hapo waliweza kukaa kambini kwa muda upatao mwezi mzima kutoka Septemba 13, 2014 mpaka mashindano hayo yalipofanyika Oktoba 11, 2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na Sitti Mtevu alinyakua taji hilo.
Redd's Miss Tanzania aliemaliza muda wake, Happiness Watimanywa akimpisha crown,Redd's Miss Tanzania wa sasa,Sitti Mtemvu.
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu, Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
Zaidi na zaidi: http://kajunason.blogspot.com/2014/10/sitti-mtemvu-ndiye-redds-miss-tanzania.html
Suala tunalozungumzia hapa baada ya kuwa tumefanya uchambuzi huko... ni kudhibitisha kwa cheti cha kuzaliwa maana leo hashimu lundega alisema kuwa jambo la msingi ambalo wanazingatia ni kila mshiriki kuwasiliasha vyeti husika vya kushiriki. Sasa hapa imeonekana Miss Tanzania, Sitti Mtemvu wakati anashiriki mashindano kuanzia ngazi ya kitongoji hakuwa na cheti cha kuzaliwa wakati alitakiwa kudhibitisha umri wake tokea ngazi ya kitongoji huku cheti kikionyesha kimetolewa 9.9.2014, tunaomba waandaaji waweze kuweka wazi ni nyaraka ipi iliyomhalalisha kushiriki mashindano haya???? tokea ngazi ya kitongoji.
Na kama mshiriki anasema cheti chake kilipotea, ni lini na wapi??? kilipotelea cheti hicho???
Toa Maoni Yako:
0 comments: