Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart,Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart,Alex Msama alipokuwa akizungumza nao mapema leo ofisini kwake,kinondoni jijini Dar, kuhusiana na mkakati wake wa kupambana na uharamia wa kazi za sanaa.
---
Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart imewaonya Wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam wanaotoa fedha kwa Wafanyabiashara Wadogo wadogo ili kupinga zoezi lakuondoa kazi feki za sanaa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema Wafanyabiashara hao waache kuwatumia Wamachinga kupinga kuondoa kazi hizo ambazo zinaikosesha Serikali mapato na Wasanii kwa ujumla.

Msama amewaasa Wafanyabiashara hao kuacha kabisa kuwatumia Wamachinga, amesema Wafanyabiashara hao watakamatwa kutokana na kuhamasisha maandamano.

Pia amewaasa Wafanyabiashara Wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga kuacha kulalamika kwani Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wananchi hao, Wafanyabiashara wanaolipa Kodi kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.

"Wamachinga acheni kulalamika, mnaopoenda kununua Filamu za nje na ndani hakikisheni Filamu hiyo ina Stika ya TRA, ukiuza yenye Stika mtu hatokukamata", amesema Msama.

Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: