Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia Magic Fm Radio kuhusu ugonjwa wa kisukari. Wataalam waliokua wakitoa mada walikua Prof. Endrew Swai na Dr Mohamed Juma. Kwa ufupi wamesisitiza sana kufanya mazoezi kwa takriban nusu saa kwa siku na ambayo mtu anatoa jasho na moyo kumwenda mbio. Hiyo ni kwa ajili ya kusaidia misuli ya miguu, tumbo kifua, mgongo na mikono kutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini.

Kadhalika wamesisitiza sana kula vyakula visivyokobolewa,ikiwamo kula dona badala ya sembe, ulezi, mtama na matunda. Watu wapunguze na ikiwezekana kuacha kunywa vimiminika vyenye sukari,ikiwamo juice, soda pombe na vinginevyo. Na hiyo nikwasababu vinywaji hivyo havikai tumboni na badala yake huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida.

Vyakula visivyokobolewa vinafaida sana kwani vinachukua muda wa kutosha kutoka kwenye tumbo na kwenda kwenye utumbo mwembamba na hatimaye kuvunjwavunjwa kwa ajili ya kutumika mwilini. Kadhalika makapi yatokanayo na hivyo vyakula hutuzuia kupata kansa ya utumbo. La ajabu wametoa takwimu za kutisha kwani ulaya kwasababu wanakula vyakula vilivyokobolewa wanapata kansa ya utumbo kuliko nchi au bara la afrika,na kansa hiyo ni ya nne kwa kusababisha vifo barani ulaya na amerika.

Tafadhalini tujihadharini kwani mada ilikua ndefu na nzuri sana kwa mustakabali wetu na afya zetu.

1.Mazoezi ni muhimu
2.Vyakula viwe na uasilia wake
3.Mtu aliye na mwenza wake afanye tendo la ndoa kwa kadiri inavuowezekana kwani ni sehemu ya mazoezi
4. Tubadili mifumo ya maisha yetu,kukaa tu bila kuishughulisha miili yetu.
Atakayeona anataka kupata elimu zaidi hao madaktari niliowataja wapo hospitali ya muhimbili kitengo cha tiba ya kisukari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: