Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, ametoa ufadhili kwa Kundi la Waandishi wa Habari wanaojishughulisha na ujasiriamali (Habari Group) kushiriki katika sherehe za kutimiza miaka kumi ya upambaji maharusi ya kampuni ya Maznat.

Kairuki ambaye pia ni mlezi wa Habari Group alitoa nafasi hiyo ya pekee kwa waandishi hao kuhudhuria sherehe hizo zitakazofanyika Mei 5 mwaka huu, Diamond Jubilee ambapo pamoja na mambo mengine itasaidia kujenga mtandao na kujifunza mambo mbalimbali katika tasnia ya ujasiriamali.

Mwenyekiti wa Habari Group, Mwanamkasi Jumbe alisema wanamshukuru kiongozi huyo, ambaye amekuwa ni msaada mkubwa kwa kikundi hicho.

Aliongeza kuwa tangu kikundi hicho kizinduliwe rasmi Machi 8 mwaka huu, wamekuwa wakipata msaada mkubwa wa ushauri na usimamizi wa karibu kutoka kwa Angellah, na kwamba ni kiongozi anayejua majukumu yake.

"Kwa sasa tunaandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama na hayo tunaanda chini ya msaada mkubwa wa Mheshimiwa Kairuki. Kuachana na mambo mengine, ni kiongozi mwenye msaada wa kipekee kwa jamii yote,"aliongeza Mwanamkazi.


Wanachama wa Habari Group kila mtu kwa nafasi yake alishukuru kwa ufadhili huo, na kwamba watatumia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya kutimiza ndoto zao za kujikwamua kiuchumi kutoka katika hali ngumu ya kimaisha.

"Kwa kuwa Habari Group pia inaanda shughuli mbalimbali, itakuwa ni fursa ya pekee kujifunza jinsi wenzetu wanavyofanya, changamoto na mafanikio, ili nasi kwa nafasi zetu tufikie malengo tuliyojiwekea,"aliongeza Katibu Msaidizi, Asha Bani.

Sherehe hiyo ya Maznat itahudhuria na wajasiliamali wa aina zote wakiwemo wa mapambo, urembo, washehereshaji katika matukio mbalimbali na wabunifu wa mitindo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: