Articles by "SIASA"
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu) Dkt. Rose Likangaga akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Dkt. Zakia Mohamed Abubakar.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu) Dkt. Rose Likangaga akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Dkt. Zakia Mohamed Abubakar.
Mwenyekiti wa Mafunzo, Bw. Khalid Khalif akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Na Mwandishi wetu, Songea
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura mkoani Ruvuma wametakiwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao baadae mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu) Dkt. Rose Likangaga wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao mkoani Ruvuma.

“Mnahimizwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao,” ilisema sehemu ya hotuba hiyo.

Dkt Likangaga akisoma hotuba hiyo alisema ni matarajio ya Tume kuwa, mara baada ya zoezi hili lililopo mbele yao kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni Wapiga Kura Halali.

Aidha alisema, jukumu la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja wao watendaji kwa kushirikiana na wadau wengine katika maeneo yao kupitia nyenzo walizonazo.

“Ninasisitiza kwamba, mabango na vipeperushi mtakavyopewa na Tume mvisambaze mapema katika kata zote zilizopo katika halmashauri zenu. Kazi yenu kubwa ni kusimamia na kuendesha shughuli zote za uboreshaji katika halmashauri zenu,”ilisisitiza hotuba hiyo.

Watendaji hao wameatakiwa kuisoma kwa umakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Sheria za Uchaguzi, Kanuni za Uboreshaji, Maelekezo na Miongozo yote inayotolewa na Tume ili kazi yao ifanyike kwa uadilifu na haki.

Pia wametakiwa kuwasiliana na Tume kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala yote yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu yao pindi wanapokutana na changamoto zozote.

“Tume imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na hivyo nanyi mna wajibu wa kuhakikisha kuwa mnatekeleza kikamilifu majukumu yote mliyokasimiwa,” ilisema sehemu ya hotuba hiyo.

Pia Tume imewataka watendaji hao kuwa makini katika kila eneo la usambazaji na utunzaji wa vifaa na muda sahihi wa ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikishia wapiga kura.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unataraji kuanza Januari 12 hadi 18, 2025 katika mikoa ya Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Mbinga Mji, Wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Mafunzo hayo yaliwahusisha Maafisa Waandikishaji,Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi, Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.


Washiriki wakisikiliza hotuba ya kufunga mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea

mmoja wa wakufunzi akitoa maelekezo wakati wa mafunzo kwa vitendo.

Washiriki wakifanya mafunzo kwa vitendo.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Kilimanjaro.


Washiriki wa mafunzo kutoka Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Arusha.
******************Na Waandishi wetu, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma
Watendaji wa uchaguzi kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dodoma leo tarehe 30 Novemba, 2024 wamepatiwa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa daftari hilo katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Kondoa Mji na Chemba. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024.

Akifungua mafunzo hayo jijini Arusha, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watendaji hao kwa sababu ujuzi na elimu watakayopata itawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kufanikisha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Mafunzo haya yanalenga kuwajengea umahiri watendaji wetu ili waweze kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata, ambao nao watatoa mafunzo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi, ambao ndio watakaohusika moja kwa moja na uandikishaji wa wapiga kura katika vituo,” amesema Jaji Mwambegele.

Pia, Jaji Mwambegele amesisitiza umuhimu wa kutumia uzoefu wa watendaji waliowahi kushiriki katika mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ili kusaidia wenzao ambao hawajawahi kushiriki katika zoezi kama hili, na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Katika mkoa wa Kilimanjaro, mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi ngazi ya mkoa yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (Mstaafu). Akizungumza katika ufunguzi, Jaji Mbarouk amesisitiza kuwa mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikishaji wapiga kura, lakini ameonya kuwa hawataruhusiwa kuingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu.

“Kwa madhumuni ya kuleta uwazi, mawakala wa vyama vya siasa watasaidia kutambua waombaji wapiga kura katika maeneo yao, jambo litakalosaidia kupunguza vurugu zisizohitajika,” amesema Jaji Mbarouk. Ameongeza kuwa ni muhimu kwa watendaji wa uchaguzi kutoa ushirikiano kwa mawakala hao na kuhakikisha maelekezo ya Tume yanafuatwa ipasavyo.

Vilevile, mafunzo hayo yalifanyika mkoani Dodoma, ambapo Mjumbe wa Tume na Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari, alifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Jaji Asina amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa vifaa vya uandikishaji, akisema kuwa kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu.

“Vifaa vya uandikishaji vimenunuliwa kwa gharama kubwa, hivyo ni lazima tuvisimamie kwa umakini na kuhakikisha vinatumika ipasavyo katika maeneo yote ya uandikishaji,” amesema Jaji Asina.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na maafisa waandikishaji, maafisa TEHAMA, pamoja na maafisa ugavi kutoka halmashauri mbalimbali za mikoa hiyo. Washiriki walipata ujuzi wa jinsi ya kutumia mfumo wa Voters Registration System (VRS) pamoja na vifaa vya kisasa vitakavyotumika katika vituo vya kuandikishia wapiga kura. Vilevile, walifundishwa namna ya kukabiliana na changamoto za kiufundi zinazoweza kutokea wakati wa zoezi la uandikishaji.

Washiriki wa mkoa wa Arusha wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo.
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji, Adrian Ntambala akiwasilisha mada kuhusu uraia kwa washiriki wa mafunzo mkoa wa Arusha.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Asina Omari akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Dodoma.



Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo yao leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Dodoma.


Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo yao leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Kilimanjaro.
Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo yao leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Kilimanjaro.
Meza kuu wakati wa mafunzo

Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo yao leo Novemba 30 hadi Disemba 1, 2024 Mkoani Arusha.
Na Oscar Assenga, TANGA.

Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Novemba 27 mwaka huu katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, vimetoa tamko la pamoja na kupongeza mchakato wa Uchaguzi huo huku vikitaka dosari chache zilizojitokeza zifanyiwe kazi na Tamisemi.

Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM),Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,vyama vyengine ni (ACT-Wazalendo) CUF, ADC,TLP na NCCR-Mageuzi.
Vyama hivyo vimetoa tamko la pamoja leo Novemba 29 mara baada ya matokeo ya jumla kutangazwa hapo Novemba 28 mwaka huu ambapo CCM katika Jiji la Tanga kimeibuka kidedea kwa kushinda viti vyote vya kuanzia wajumbe na wenyeviti wa mitaa yote.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa tamko la pamoja,Mussa Mbarouk ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wilaya ya Tanga alisema kwamba uchaguzi ulifanyika kwa njia ya amani japo kulikuwa na dosari ndogondogo ambazo wanaamini zitafanyiwe kazi,

"Mchakato wa Uchaguzi huu ulienda vizuri, tulikuwa tukishirikiana na Serikali ya Mkoa na Jiji, kulikuwa na dosari ndogondogo lakini hata sisi vyama vya siasa tunatakiwa tukae na tuungane ili yale maeneo yote yenye Wagombea wanaokubalika tumuunge mkono" Alisema Mbarouk.
Mbarouk alisema kwamba chama chake pamoja na vyama vyote shiriki katika Uchaguzi huo vimesikitishwa na matokeo ya jumla ambapo hakuna chama cha upinzani kilichoshinda kiti hata kimoja.

"Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2019 tulipata walau viti 61,lakini safari hii haijawahi kutokea kiukweli ni lazima tujipange vizuri Uchaguzi Mkuu Ujao mwaka 2025" Alisisitiza Mbarouk.

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Chadema Hemed Bakari alisema kuna umuhimu mkubwa kwa vyama vya siasa kuongeza nguvu ya ushawishi kwa wapiga kura.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tang Shaban Kalaghe alisema mchakato wa Uchaguzi huo ulienda vizuri na kuwashukuru watu wote waliojiandikisha na kupiga kura,

“Kwa kweli niwapongeze wasimamizi wa uchaguzi huu ulienda vizuri tulikuwa na wagombea kwenye mitaa yote na tumeshinda kwa asilimia 100 lakini pia tunawashukuru wenzetu wa vyama vingine kwakukubali matokeo ni jambo zuri na linaonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa”Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba uchaguzi huu umeisha na sasa wanakwenda kufanya kazi lakini pia kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Arusha ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.


Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Rufaa (Mstafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Rufaa(Mstafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024.



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Arusha ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchagizi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani.
Mjumbe wa Tume Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akifuatilia mada wakati wa mkutano.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw.Stansalaus Mwita akiwasilisha mada ya Mfumo wa Uboreshaji wa Daftari katika mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Daftari na TEHAMA (Daftari), Bw. Martin Mnyenyelwa akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wadau kuhusu mfumo wa uboreshaji kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi Giveness Aswile akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, wakati wa mafunzo kwa wadau kuhusu mfumo wa uboreshaji kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za kisheria wa INEC, Bw. Selemani Mtibora akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau mkoani Kilimanjaro.


Wadau wa uchaguzi kutoka Mkoani Kilimanjaro wakiwa mkutano wa wadau.
Wadau wa uchaguzi kutoka Mkoani Arusha wakishiriki mkutano wa Tumen a Wadau wa Uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.


Na Mwandishi Wetu.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Arusha na Kilimanjaro utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024.

Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkaoni Arusha leo tarehe 29 Novemba, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huo pia utajumuisha Mkoa wa Dodoma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Amesema mikoa hiyo inafanya uboreshaji wa Daftari ikiwa ni mwendelezo wa zoezi hilo ambalo lilizinduliwa tarehe 20 Julai, 2024 mkaoni Kigoma.

Akifungua mkutano kama huo mkoani Kilimanjaro, Makamu Mweneyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk amesema zoezi hilo tayari limeshafanyika Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida na Zanzibar.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan amesema Tume imeridhia kuongezeka kwa vituo 44 vya kupigia kura ambavyo vinafanya idadi ya vituo vya kupigia kura nchini kuwa 40,170 kutoka 40,126 vilivyokuwepo awali.

“Tume imeridhia kufanyika kwa mabadiliko ya idadi ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kutoka vituo 40,126 hadi kufikia vituo 40,170 kwa kurejesha vituo 44 vya Kata 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Vituo 39,753 vipo Tanzania Bara na 417 vipo Zanzibar,” amesema.

Hatua hiyo ya Tume imetokana na amri ya Waziri wa Nchi, mwenye dhamana ya TAMISEMI kupitia Tangazo la Serikali Na. 796 ya tarehe 06 Septemba, 2024 ambayo pamoja na mabadiliko mengine, imerejesha kata 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ambazo zilifutwa hapo awali.

Kailima amesema kwenye Mkoa wa Arusha Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 224,499 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 ya wapiga kura 1,255,584 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Ameongeza kuwa Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Arusha utakuwa na wapiga kura 1,480,083.

Amesema kwa Mkoa wa Arusha kuna vituo 1,454 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 86 katika vituo 1,368 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Akiwasilisha nada mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume, Bw. Selemani Mtibora amesema kwa mkoa wa Kilimanjaro Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 180,540 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 ya wapiga kura 1,009,726 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Kilimanjaro utakuwa na wapiga kura 1,190,266,” amesema.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una vituo 1,316 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 30 katika vituo 1,286 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Wadau wa uchaguzi kutoka Mkoani Arusha wakishiriki mkutano wa Tumen a Wadau wa Uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.