Articles by "NAFASI ZA KAZI"
Showing posts with label NAFASI ZA KAZI. Show all posts
Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K.Mutungi akionyesha kitabu chenye kuelimisha uma juu ya makatazo yaliyomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Mafunzo ya Watumishi yaliyofanyika leo Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Bi. Piencia Kiure, Msajili Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma akitoa mwongozo wa namna sahihi ya ujazaji wa fomu za gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vya siasa ambazo hubainisha mapato na matumizi wakati wa uchaguzi.
Mwanasheria Mwandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bi. Monica Mwailolo , mmoja wa wakufunzi akiwakilisha mada wakati wa mafunzo.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyaa vya siasa wakati wa Mafunzo

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa ofisi yake ili kuwajegea uwezo wa kufanya uangalizi wa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018 katika jimbo la Buyungu na kata 79.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo mada juu ya Elimu ya Maadili ya Vyama vya Siasa, Haki na wajibu wa Vyama vya Siasa, wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa, matendo yanayokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa, Umuhimu wa kujaza fomu za gharama za Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amewawataka watumishi hao kufanya kazi kwa ueledi na kwa kufuata sheria za nchi.

“ kila mmoja wetu atambue kuwa ofisi yetu imepewa dhamana kubwa ya kusimamia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kudumisha demokrasia ya vyama vingi nchini, ni wajibu wetu kufanya kazi kwa ueledi na kwa mujibu wa sheria” amesisitiza Jaji Mutungi

Naye Bi. Piencia C. Kiure mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo ambaye ni Msajili Msaidizi anayeshughulika na masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma amesisitiza umuhimu wa wagombea na vyama vya Siasa kurejesha fomu za Gharama za uchaguzi zinazobainisha mapato na maksio ya kiwango cha matumizi wakati wa uteuzi,kampeni na uchaguzi ndani ya muda uliotengwa kisheria ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Watumishi pia wamesisitizwa kuhakikisha wanavikumbusha vyama vya siasa na wagombea kunadi sera za vyama vyao kwa kusimamia maadili ya vyama vya siasa ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni taasisi yenye wajibu wa kisheria wa kufanya uangalizi wa mwenendo wa chaguzi zinazofanyika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wagombea na vyama vya siasa vinatekeleza matakwa ya sheria kwa kuepuka vitendo ambavyo vimekatazwa na sheria hizi ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.

Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla Akiwa anamtunuku mmoja wa mwanafunzi wa shahada ya uzamini aliyejulikana kwa jina la Anna

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru wakiwa wanajiself na naibu waziri mara baada ya mahafali hayo kumalizika

Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi shuleni hapo waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri pamoja na bodi ya chuo hicho.


Naibu waziri akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mahafali kumalizika wa kwanza kulia
ni Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki wakwanza kushoto ni kaimu mwenyekiti wa bodi ya taasisi hiyo Dr. Rosemarie Mwaipopo.

Wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha.


Wakwanza kushoto ni mkuu wa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru Anatory Bunduki akiteta jambo na Naibu waziri Kigwangala.





Na Woinde Shizza, Arusha.

Serikali inajipanga kuajiri maafisa ustawi wa maendeleo ya jamii 5,554 kwakipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya kata na vijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa awamu ya kwanza nchini.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla alipokuwa akihutubia katika mahafali ya sita katika fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji la Arusha.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata hivyo ilisaidia kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka zaidi na kutoa ushauri wa miradi mbalimbali inayowazunguka wananchi haswa wa vijijini.

“Katika serikali ya awamu ya kwanza maafisa ustawi wa jamii walikuwa wapo hadi vijijini unakuta bibi ustawi wa jamii na babu ustawi wa jamii kitu ambacho kwa kipindi cha nyuma hapa kilipotea kabisa sasa serikali hii ya awamu ya tano tunataka kurudisha icho kitu” alisema Kigwangala.

Alivitaka vyuo mbalimbali vinavyofundishia kozi ya ustawi wa jamii kuakikisha wanaongeza idadi ya wataaalamu wanaosomea ustawi wa jamii ili kuweza kupunguaza tatizo hili kwani kwa sasaivi kadri siku zinavyozidi kwenda ndivo wanafunzi wanaosomea ustawi wa jamii wanapungua.

“Kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii wameanza kupungua sana na ivyo kila chuo kinatakiwa kuongeza idadi ya wa wanafunzi ili kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu wa maendeleo ya jamii kila wilaya, kata na hata kijiji.

Kigwangala alitoa wito kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa elimu yenye
viwango bora na wazingatie katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu.

"Napia napenda kusema kuwa hao wamaafisa ustawi wa jamii wasome kabisa wakijua serikali itawaajiri sawa lakini wasitegemee watakaa ofisini tu au katika ofisi za halmashauri apana wajue kabisa wataenda kufanya kazi vijijini ili waweze kutambua matatizo ya wananchi na kuyatatua pamoja nakuvumbua miradi mbalimbali ya jamii itakayosaidia wananchi "alisema Kigwangala.

Alisema Nchi itabadilika sanamna kuwa na maendeleo ikiwa wanataaluma wa Nchi hii wataipenda Nchi yao kama ambavyo kila mtu ampendavyo mama yake nakujituma sana katika utendaji kazi utaendana na falsafa ya hapa kazi tu.

Kwa upande wake Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki akisoma hutuba wakati Mahafari hayo alisema kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kufanya tafiti za kina kwa masuala ya wanawake, jinsia, watoto wa kike ili kuwainua kiuchumi, kisiasa,kiutamaduni na kijamii na kuzitumia tafiti hizi kujadili katika kuandaa sera na kutoa maamuzi yanayojumuisha amsuala ya kijinsia katika kutekeleza sera mbalimbali hapa Nchini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza na wakazi wa Kawe kuhusu kampeni ya VIWANDA NI FURSA.

Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akieleza wakazi wa Kawe jinsi wanavyoweza kubadili maisha yao kwa kufanya biashara na jinsi kampuni yake ya HiTECH inaweza kuwapa mkopo.

Diwani wa Kawe, Ruta Rwakatare akimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri kwa jinsi ambavyo amejitoa kusaidia wajasiliamali ambao wanataka kufanya biashara kwa kuwapatia mashine kwa mkopo wa bei nafuu.

Baadhi ya watu waliohudhuria semina hiyo wakitoa maoni na kuuliza maswali.



Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Kata ya Kawe waliohudhuria semina hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya HiTECH International.

Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda, Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri ameanzisha kampeni mpya ya VIWANDA NI FURSA ambayo itatoa elimu kwa wananchi pamoja na kutoa mikopo ya mashine za viwanda vidogo vidogo kwa wajasiliamali.


Akielezea kampeni hiyo wakati akifanya semina kwa wakazi wa Kawe, Mashauri alisema kuwa ameanzisha kampeni hiyo ili kutoa elimu kwa wananchi lakini pia kuwapa mikopo ya mashine kwani watu wengi wanatamani kufanya biashara lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukosa mtaji wa kufanya biashara.


Alisema kuwa ili nchi kuwa kufanikiwa kwa kuwa na uchumi mkubwa na kuwa na maendeleo kwa wananchi wake ni lazima iwe na viwanda vingi ili kuwepo ajira za kutosha na shughuli za maendeleo hivyo kupitia kampeni hiyo itaweza kubadili maisha ya watanzania wengi ambao tayari walikuwa wameanza kupoteza matumaini ya kufanikiwa kimaisha.

"Kampuni ya HiTECH imeanzisha kampeni hiI na itafanyika nchi nzima, serikali tayari imekubali tuifanye kimechobaki ni wananchi wenyewe, tutatoa mikopo ya mashine kwa watakaohitaji na watarudisha kwa riba ndogo ya asilimia 10,

"Ukienda nchi ambazo zimeendelea kama China kuna viwanda vingi, na watu wanajua kiwanda mpaka uwe na eneo kubwa wakati watu hata majumbani wana viwanda na wanazalisha, ni muda sasa watanzania kuchangamkia nafasi hii ambazo HiTECH International imeitoa," alisema Mashauri.

Nae Diwani wa Kawe, Ruta Rwakatare alimpongeza Mashauri kwa uamuzi wa kutoa mikopo kwa wananchi ambao wana malengo ya kufanikiwa kwa kufanya biashara na anaamini kuwa hiyo itakuwa njia moja wapo ya kumaliza vijiwe vya vijana ambao hawafanyi kazi.


"Mimi sipendelei kuona vijana wanakaa tu vijiweni, na sio kwamba wanapenda ila tu sababu hakuna kazi lakini kupitia kampeni ya Paul Mashauri itaweza kuwasaidia kuacha tabia hizo na kuanza kufanya kazi zinazowaletea maendeleo.

"Nchi yetu kwa sasa tunataka kupiga hatua kwa kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda kama anavyosema rais wetu, na hilo muda wa kuwa na viwanda ni sasa na tunaanza na viwanda vidogo vidogo ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wetu," alisema Rwakatare.
 MBUNIFU wa Mavazi Manju Msita anatoa nafasi za kazi kwa mafundi wa kushona (tailors) wenye uwezo mkubwa wa kutumia akili zao kufanya kazi nae...

Wawe na umri kati ya miaka 22-35. 

Ni fursa ya pekee na pia changamoto kwa wale wanaopenda kuongeza uwezo wa kufikiri na kujiamini katika kazi zao.

Wanatakiwa mafundi wenye uzoefu wa miaka mitatu na kuendelea na wenye uwezo wa kushona nguo za kike na za kiume zikiwemo suti watafikiriwa zaidi.

Wasiliana nasi kwa namba 0766/0655 (411441).