Meneja Mauzo wa Vodacom eneo la Makambako mkoani Njombe, Elly Mwambene (kulia), akikabidhi kapu la sikukuu kwa mmoja wa wateja wao Sigfrid Lomanus Chaula (kushoto), katika muendelezo wa kampeni ya “Tupo Nawe Tena na Tena” inayolenga kugawa makapu kwa wateja katika msimu huu wa sikukuu. Kampeni hiyo imeendelea kugawa makapu hayo katika mikoa mbalimbali nchini, Tukio hili limefanyika kwa lengo la kusherehekea pamoja na wateja katika msimu huu wa sikukuu, sambamba na kuhitimisha maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom tangu kuanzishwa kwake hapa nchini, na limefanyika mjini Makambako mwishoni mwa wiki.Na Mwandishi Wetu.
Makambako, Njombe – Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kuonyesha shukrani kwa wateja wake kwa kugawa makapu ya sikukuu katika mikoa mbalimbali nchini kupitia kampeni yake ya “Tupo Nawe Tena na Tena”, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea msimu wa sikukuu na kuhitimisha maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo hapa nchini.
Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Makambako mkoani Njombe, ambapo Meneja Mauzo wa Vodacom eneo la Makambako, Bw. Elly Mwambene, alikabidhi kapu la sikukuu kwa mmoja wa wateja wa kampuni hiyo, Sigfrid Lomanus Chaula, kama ishara ya kuthamini uaminifu wa wateja wao.
Akizungumza katika tukio hilo, Bw. Mwambene alisema kampeni ya “Tupo Nawe Tena na Tena” inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Vodacom na wateja wake kwa kusherehekea pamoja nao katika msimu wa sikukuu, huku ikionesha namna kampuni inavyojali na kuthamini mchango wa wateja katika safari yake ya mafanikio.
“Kampeni hii ni sehemu ya shukrani zetu kwa wateja waliotuwezesha kufikisha miaka 25 ya huduma nchini. Tumekuwa pamoja nao katika nyakati zote, na leo tunaendelea kuonyesha kuwa Vodacom ipo karibu nao, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu,” alisema Mwambene.
Aliongeza kuwa kampeni hiyo inaendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo makapu ya sikukuu yanagawiwa kwa wateja ili kuwaletea furaha na kuimarisha mshikamano katika jamii.
Kwa upande wake, Sigfrid Lomanus Chaula, aliyepokea kapu hilo, aliishukuru Vodacom kwa kuwakumbuka wateja wake na kuonesha kuguswa na mahitaji ya jamii, akisema hatua hiyo inaongeza imani na uaminifu kwa kampuni hiyo.
Kampeni ya “Tupo Nawe Tena na Tena” pia inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom Tanzania tangu kuanzishwa kwake, ambapo katika kipindi hicho kampuni imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mawasiliano, uchumi wa kidijitali na huduma za kijamii nchini.
Kupitia kampeni hiyo, Vodacom imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwa mshirika wa kweli wa Watanzania, si tu katika huduma za mawasiliano, bali pia katika nyakati za kusherehekea na kushirikiana na jamii.





Toa Maoni Yako:
0 comments: