Dar es Salaam Desemba 24 2025: Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam limetangaza kuwa Kardinali Mstaafu wa Jimbo hilo, Kardinali Polycarp Pengo, anakabiliwa na changamoto za kiafya na anatarajiwa kusafiri kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Askofu Thaddaeus S. Ruwa’ichi OFMCap, Kardinali Pengo amekuwa akipatiwa matibabu nchini kwa muda, hata hivyo hali yake imehitaji huduma za kitaalamu zaidi zitakazopatikana nje ya nchi.

“Baada ya juhudi za kimatibabu hapa nyumbani, imeonekana kuwa kuna haja ya kumpa matibabu ya hali ya juu zaidi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa Desemba 24, 2025.

Kanisa limeeleza kuwa mipango yote ya safari na matibabu imekamilika, na kwamba Kardinali Pengo atasafiri kwenda India kwa lengo la kupata huduma bora zitakazomsaidia kurejea katika hali njema ya afya.

Aidha, waumini na watu wote wenye mapenzi mema wametakiwa kuendelea kumuombea Kardinali Pengo ili Mungu amjalie nafuu ya haraka na kumrejesha salama nchini.

Katika taarifa hiyo, Askofu Mkuu pia ametumia nafasi hiyo kuwatakia waumini wote Heri ya Krismasi na Baraka za Mwaka Mpya 2026, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na sala katika kipindi hiki.

Taarifa hiyo imesainiwa na Askofu Thaddaeus S. Ruwa’ichi OFMCap pamoja na Katibu Mkuu wa Jimbo, Padre Vincent Mjwaji.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: