Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mbeya kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia wananchi kwa moyo wa kujituma.

Akizungumza leo, Oktoba 22, 2025, wakati akikabidhi pikipiki 12 kwa maafisa hao, Mdemu alisema serikali imetoa vyombo hivyo vya usafiri ili kuwawezesha kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi, hasa vijijini.

“Tunataka kuona pikipiki hizi zikitumika vizuri. Zitasaidie kuwafikia wananchi kwa haraka na kutatua changamoto zao kwa wakati,” alisema Mdemu.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Anna Mwambene, aliishukuru Wizara kwa msaada huo na kusema utarahisisha kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

“Tunaomba Wizara iendelee kuwasaidia maafisa zaidi kwa kuwapatia vitendea kazi kama hivi, kwani wengi wao wanasafiri umbali mrefu kuwahudumia wananchi,” alisema Mwambene.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Mbeya, Elukaga Mwaikasu, aliwataka maafisa waliopokea pikipiki hizo kuzitunza na kuzitumia kwa kazi za maendeleo ya jamii pekee, akionya kuwa watakaotumia vibaya watachukuliwa hatua.

Maafisa waliopokea pikipiki hizo waliishukuru Serikali kwa msaada huo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi katika kuwahudumia wananchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: