Mtaalamu wa mafunzo na vijana kutoka Vodacom Tanzania Plc,Bw Samwel Komba akimkabidhi cheti Mwanafunzi Doris Nisetasi, mhitimu wa mafunzo ya programu ya 'Code Like A Girl' yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ambayo inafadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika ijumaa jijini Dar es Salaam
Mwanafunzi wa programu ya Coding, Lairati Yahya, akiwakilisha mradi wa kundi lake wakati wa kilele cha mafunzo ya Code Like a Girl yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Programu hii inaendeshwa na dLab kwa udhamini wa Vodacom Tanzania PLC, ikilenga kuwaelimisha na kuwahamasisha wasichana kujiunga na masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM). Hadi sasa, zaidi ya wasichana 3,370 wamehitimu mafunzo haya nchini.
Na Mwandishi Wetu.
Dar-es-Salaam, Septemba, 12, 2025, Vodacom Tanzania ikishirikiana na D Lab imewapa vyeti wasichana walioshiriki Program ya Code Like A Girl. Ambapo mpaka sasa mabinti zaidi ya 3370 nchini wamehitimu kwenye program hiyo inayolenga kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM)
Akizungumza na wanahabari mtaalamu wa mafunzo na vijana kutoka Vodacom Tanzania Plc,Bw.Samwel Komba amesema lengo ni kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike Katika masomo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) ambapo wasichana wanajfunza mambo mbali mbali ikiwemo kutengeneza website na siku ya leo wamewakilisha kile ambacho wamejifunza na kukionyesha.
Nae mmoja wa wanafunzi aliyehitimu mafunzo hayo Kurthum Hassan ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu amesema kuwa amefurahi kwa Kampuni ya Vodacom Tanzania kuwapatia mafunzo hayo kwa sababu wamepata kujifunza namna ya kutumia Komputa kwa undani zaidi kupitia mafunzo ameweza kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo kutengeneza website na kuposti vitu mbalimbali.




Toa Maoni Yako:
0 comments: