Meza kuu wakifuatilia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazalishaji Maudhui Mtandaoni wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa Tume Huru wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

LMwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazalishaji Maudhui Mtandaoni wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa Tume Huru wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazalishaji Maudhui Mtandaoni wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa Tume Huru wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazalishaji Maudhui Mtandaoni wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa Tume Huru wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazalishaji Maudhui Mtandaoni wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa Tume Huru wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, ametoa wito kwa wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuhakikisha taarifa wanazopandisha kwenye mitandao yao zinakuwa sahihi na zisizo na chembe ya upotoshaji, ili kulinda amani na utulivu wa taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza leo, Agosti 3, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kitaifa kati ya INEC na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni, Jaji Mwambegele alisisitiza umuhimu wa kutumia majukwaa ya kidigitali kwa uadilifu na weledi, hususan wakati huu wa maandalizi ya uchaguzi mkuu.

“Nawasisitiza na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kuepuka matumizi mabaya ya akili unde (Artificial Intelligence), ambayo hutumiwa vibaya na baadhi ya watu kusambaza habari za upotoshaji, hasa kupitia mitandao ya kijamii,” alisema.

Ameeleza kuwa Tume ina matumaini makubwa na vyombo vya habari na watengenezaji wa maudhui katika kufanikisha uchaguzi kwa njia ya uwazi na utulivu, kutokana na ushirikiano wao uliotukuka katika hatua za awali, ikiwemo zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Mmekuwa wepesi kuwasilisha hoja na ushauri pale inapohitajika, jambo linaloonesha utayari wenu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi,” aliongeza Jaji Mwambegele.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ramadhan Kailima, akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi, alisisitiza wajibu wa vyombo vya habari na watayarishaji wa maudhui kuwa mabalozi wa amani na uwazi katika kipindi chote cha uchaguzi.

“Tunaomba na kuwasihi kutumia nafasi mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo taarifa za mara kwa mara kuelezea kinachoendelea kuhusu uchaguzi. Kalamu zenu ni silaha ya haki na sauti ya ukweli,” alisema Kailima.

Aidha, Kailima alibainisha kuwa Tume imeweka utaratibu wa kuvishirikisha vyombo vya habari na wazalishaji wa maudhui katika kila hatua ya uchaguzi ili kuimarisha uwazi, kuondoa upotoshaji na kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwa njia salama na yenye tija.

Mkutano huo umetajwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa INEC wa kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 unakuwa wa amani, huru na wa haki, huku ikisisitiza kuwa habari zenye mizizi ya ukweli ni silaha muhimu ya kulinda demokrasia ya taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: