Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Mhe. Ussi Salum Pondeza, ameshiriki ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Abiria Maruhubi, mradi wa kimkakati unaolenga kuimarisha sekta ya usafirishaji na kukuza uchumi wa nchi.
Mhe. Hemed amesema kukamilika kwa bandari hiyo kutasaidia kupunguza msongamano wa abiria na mizigo katika Bandari ya Malindi, pamoja na kuchochea ukuaji wa biashara visiwani.



Toa Maoni Yako:
0 comments: