Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus. Dkt. Constantinos Kombos amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini Tanzania na kuagwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam Julai 10, 2025.

Wakati wa ziara yake nchini, Dkt. Constantinos Kombos alikutana na viongozi mbalimbali akiwemo mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ambapo kwa pamoja walisaini Hati ya Makubaliano Kuhusu Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Cyprus ambayo yanatarajiwa kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: