Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania PLC, Athumani Mlinga akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa washiriki wa programu ya ‘Code Like A Girl’ katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo jijini Dar es Salaam. Programu hii inalenga kuwawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 kwa kuwapa ujuzi wa kidijitali na kuwaandaa kwa mustakabali wa masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).
Mmoja wa wahitimu akifanya wasilisho la mradi wa kundi lake katika kilele cha mafunzo ya Tehama (Code like a Girl) jijini Dar es Salaam. Mradi huo unaendeshwa na taasisi ya dLab kwa udhamini wa Vodacom Tanzania PLC, ikilenga kuwajengea wasichana ujuzi wa TEHAMA na kuwahamasisha kupenda masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: