Na Oscar Assenga, TANGA
MABALOZI 23 wa Mkoa wa Tanga unaoundwa na Wasanii wa Filamu,Waandishi pamoja na watangazaji wametua Jijini Tanga kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Kupiga kura .
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Ramadhani Omary alisema wameamua kujikusanya kwa pampoja kuja mkoani kwao kuleta hamasa kwenye dafrati la kudumu la wapiga kura.
Alisema kwamba watu wanapozungumzia mkoa wa Tanga hawawezi kuacha kuitaja Bandari,Zao la Mkonge ,Reli na Viwada na ukiangalia Bandari,Reli ndio ina hudumia viwanda na Rais Dkt Samia Suluhu ameweka fedha nyingi kwa ajili ya upanuzi kwenye Bandari ya Tanga .
Aidha alisema pia mkakati wa kuiboresha reli kuelekea mkoa wa Arusha na ambao itaifungua mkoa wa Tanga na serikali ina mkakati baada ya ubinafsishaji wale watu ambao hawakuviendelea viwanda vitarudi chini ya Serikali.
“Waliposikia Rais Dkt Samia Suluhu anatarajiwa kuja Tanga nao wakaamua kuja nyumbani kumpokea tutashiriki kwenye maandalizi na tutakuwepo Tanga muda wote mpaka Rais atakapowasili na leo tumeona tuhabarisha umma kupitia nyie wanahabari”Alisema
Awali akizungum za Chuchu Hans alisema kwamba wameungana na mabalozi wa Tanga na wao ni watu wa kujituma wana vipaji vingi ikiwemo ukarimu na wao wanawakilisha wenzao.
“Tumeona ni muda sahihi na umefika wakati wa kujiandikisha na tukaona tutumia nafasi hii kuhamasisha wananachi na sisi kuja kujiandikisha kwenye Daftari lakini pia Rais anakuja”Alisema.
Hata hivyo aliwaomba wananchi amba bado hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupigia kura wakajiandikishe vituo vyote vipo wazi hivyo watumie haki yao ya msingi kwa ajili ya baadae kuwachagua viongozi wao.
Awali akizungumza katika mkutano huo na wanahabari Salim Awadhi “Gabo”- alisema wao wamekuja kuwakilisha wenzao kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema kwasababu mkoa wa Tanga ni watu wa ukarimu wao wameliona wabebe jukumu hilo kumsaidia Mkuu wa Mkoa huo Balozi Batilda Burian ambaye amekuwa kinara wa maendeleo kwenye mkoa huo.
Hata hivyo kwa upande wake Maliki Bandawe ambaye ni Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la TNG alisema wameamua kurudia Tanga ili kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura lakini pia kutoa hamasa na kuwakumbusha vijana kujiandikisha kwenye daftari hilo.
“Wana Tanga tujitokezeni kwenye mapokezi ya Rais Dkt Samia Suluhu anakuja kwa mara ya kwanza baada ya kupitishwa na CCM kuwa Mgombea Urais kwenye uchaguzi Mwaka huu 2025”Alisema
Akielezea malengo ya ziara hiyo, Kiongozi wa Msafara Khalidi Swalehe alisema msafara huo mabalozi 23 kutoka mikoa tofauti wote ni wazawa wa mkoa wa Tanga ambao wanaitumia kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na mapokea ya kumlaki Rais Dkt Samia Suluhu.
“Naombeni wakazi wa Tanga waunge mkono na tulichokuja kukifanya ni kuhamasisha watu kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la kupiga kura na kuhakikisha tunaunga mkono jitihada za maendeleo kwa mkoa wa Tanga zinaofanywa na Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda akimuwakilisha Rais Dkt Samia”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba mkoa huo umeendelea kuamka kwa maana Tangu Tanzania ipate uhuru ilikuwa inasifika na kuna miradi mingi ya maendeleo imefanywa na Rais Dkt Samia Suluhu na wao wanahamasisha yale yanayopaswa kwenda masikioni mwa watu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: