Na Mwandishi Wetu, Manyara.

Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imeshiriki na kudhamini Matembezi maalumu ya kuhamasisha Wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura yanayofahamika kama "Manyara Daftari Day " ambapo Mamia ya wakazi wa mkoa wa Manyara wameshiriki wameshiriki matembezi hayo yaliyofanyika katika viwanja ya Tanzanite Kwaraa Stedium.

Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi ya Kilomita 4.4 yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga .Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wamedhamini matembezi hayo ili kuhamasisha Wananchi kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka.

Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo ni scheme ya Jamii na imekua ikounga mono shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo matembezi hayo ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbali mbali ili kupata viongozi bora watakaoleta maendeleo kuanzia ngazi ya mtaa,vijiji,kata,jimbo na Taifa.

"Tumeanza kuhamasisha vijana kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapira kura hata kwenye viwanda vyetu kuhakikisha kuwa wanajiandikisha na ikiwapendeza wanaweza kuweka kituo maalumu karibu na kiwanda chetu ili vijana wengi waweze kujiandikisha" Anaeleza Mulokozi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura litakaloanza Septemba 4 hadi 10 mwaka huu huku likisimamiwa vyema na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: