Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Vodacom Business Nguvu Kamando (wa pili kushoto) wakionesha tuzo walizoshinda katika wiki ya ubunifu iliyoambatana na utoaji wa tuzo za Tanzania Digital Awards ambapo Vodacom iliibuka kidedea kwa kunyakua tuzo tano.
---
KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini ya Vodacom, imetunukiwa tuzo na Kampuni ya Serengeti bytes kupitia programu ya Tanzania Digital Awards katika wiki ya ubunifu (Innovation week).
Kampuni hiyo ya Vodacom imejishindia tuzo katika vipengele vitano ambavyo ni:


Kampuni bora ya simu nchini
Kampuni ya simu inayotoa huduma bora zaidi nchini
Applikesheni bora ya huduma za kifedha
Tuzo ya ubunifu wa kidijitali katika Afya (m-mama)
Tuzo ya ubunifu wa kidijitali katika sekta ya huduma za kifedha (M-Koba)
Mkurugenzi wa Vodacom Business Nguvu Kamando (kushoto) akipokea tuzo ya kampuni bora ya simu iliyotolewa na kampuni ya Serengeti bytes na kupigiwa kura na Watanzania.
Mkuu wa idara ya Masoko wa Vodacom Business Aileen Meena (kulia) akipokea tuzo ya kampuni ya simu inayotoa huduma bora kwa Wateja hapa nchini.
Meneja wa mifumo mipya ya huduma za kifedha Brenda Msola (kushoto) akipokea tuzo ya kampuni ya ubunifu wa applikesheni bora ya huduma za kifedha.
Meneja wa mifumo mipya ya huduma za kifedha Brenda Msola (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa kidijitali katika sekta ya huduma za kifedha (M-Koba).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: