Aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, 13292224 Peter Msigwa amejiondoa kutoka chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Jumapili, Juni 30, 2024, jijini Dar Es Salaam.

Msigwa amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza uhalali wa kuwa mkosoaji wa CCM, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuiongoza nchi na kuwatumikia Watanzania. Pia baada ya kuchoshwa na siasa za uongo, unafiki na kiulaghai zinazofanywa na Chadema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: