● Pesa zitatumika kujenga minara mipya 200 na kuongeza upatikanaji wa huduma ya mawasiliano vijijini

● Upanuzi wa miundombinu utaboresha upatikanaji wa mtandao, na kuongeza nguvu kwenye jitihada za serikali za kufikia malengo ya kidijitali, huduma jumuishi za fedha pamoja na kutoa nafasi za ajira

Dar es Salaam, 20 May 2024: TowerCo of Africa Tanzania (TOA Tanzania), kampuni inayoongoza kutoa huduma ya miundombinu kwa kampuni za mitandao ya simu imesaini makubaliano na taasisi ya Uingereza, British International Investment (BII) ambapo kampuni hiyo ya Uingereza imetoa dola za kimarekani milioni 30 zitakazotumka kupanua miundombinu ya mawasiliano nchini Tanzania.

Uwekezaji huu utawezesha TOA Tanzania kujenga minara mipya 200 nchini Tanzania na kufanikisha adhma yake ya kuongeza ujumuishi wa kidijitali Tanzania.

TOA Tanzania, kampuni iliyoanzishwa February 2023, imejikita kwenye kumiliki na kutoa huduma ya kupangisha minara ya simu kwa makampuni ya mitandao ya simu. Minara mipya 200 itakayojengwa kutokana na uwekezaji huu itasaidia kuongeza upatikanaji wa mawasiliano Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar hivyo kuwaungasnisha watanzania ambao walikua mbali na huduma ya mawasiliano, hivyo unatarajiwa kuboresha maisha ya watanzania 600,000.

Innocent Mushi, Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania, alisema, "Makubaliano haya ya uwekezaji wa fedha na BII yatatuongezea nguvu ya kufikia malengo yetu ya kupanua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuongeza kasi ya kukua kwa huduma za kidijitali Tanzania. Kwa hisani ya BII tunaweza kukuza upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kimtandao kwenye jamii zilizokuwa mbali na huduma hizo. Tumejidhatiti kwenye mazingira endelevu na maendeleo ya jamii. Utengenezaji wa saiti zetu mpya utazingatia utunzaji wa mazingira, matumizi ya nishati jadidifu na utupaji wa taka salama.”

Akizungumzia ushirikiano kati ya TOA Tanzania na BII, Richard Palmer,muwakilishi wa BII, said, “Upanuzi wa miundombinu ya kidijitali ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya uchumi Tanzania. Kwa kujikita kwenye maeneo ya vijijini, TOA Tanzania imedhirisha kujiidhatiti kwenye ujumuishwaji na kuhakikisha kuwa maeneo yaliyoachwa mbali na huduma za kidijitali yanajumuishwa. Tumefurahi kushirikiana na TOA Tanzania kufanikisha maono yetu ya kuboresha sekta ya mawasiliano na kufanikisha jamii iliyowezeshwa kidijitali.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, alisema“tumefurahi kushuhudia usainiwa wa makubaliano haya muhimu kwa BII ambayo yatawezesha upanuzi wa huduma za mawasiliano na kufikia watanzania wa maeneo ya vijijini. BII ni sehemu muhimu ya jithada za Uingereza za kukuza uwekezaji Tanzania, na uwekezaji huu unasapoti makubaliano kati ya Tanzania na Uingereza yaani UK-Tanzania Mutual Prosperity Partnership.”

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: