Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni, akifungua kikao cha wadau na wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mtwara Machi 22, 2024.

Na Mwandishi Wetu, Mtwara.

WADAU wa Afya wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mtwara wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, ili ziwawezeshe kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa hizo katika maeneo yao.

Akifungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni amesema uwepo wa takwimu sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za afya na kuboresha upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, amewashauri MSD kuhakikisha utaratibu wa vikao vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa pande zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia utatuzi.

Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay ameeleza kuwa kwa sasa kanda ya MSD Mtwara inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 631, na inasambaza bidhaa za afya kila baada miezi miwili.

Naye Meneja Huduma kwa Wateja na Miradi Dkt. Pamella Sawa ameeleza kuwa vikao vya MSD na wadau wake kuanzia sasa vitakuwa endelevu kila mwaka.

MSD Kanda ya Mtwara inahudumia mikoa ya Lindi,Mtwara na Wilaya ya Tunduru.Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay, akizungumza kwenye kikao hicho
Wadau wa MSD wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wadau wa MSD Kanda ya Mtwara wakifuatilia mada kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: