Mkurugugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima, akizungumza jijini Dodoma leo Juni 14,2023 wakati akitangaza taarifa ya uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 14 za Tanzania bara.
---
Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Uchaguzi
Mdogo wa Udiwani katika Kata 14 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 13 Julai mwaka
2023.
Akitangaza Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma leo,
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema
uchaguzi huo unafanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye
dhamana ya Serikali za Mitaa.
Amefafanua kuwa Waziri ametoa taarifa hiyo
kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali
za Mitaa, Sura ya 292.
“Kutokana na taarifa hiyo, Tume kwa
kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za
Mitaa, Sura ya 292, inatoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo
wa adiwanikatika kata 14 za Tanzania
Bara”alisema Kailima.
Kailima amezitaja kata hizo kuwa ni Kata ya
Ngoywa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Kata ya Kalola iliyopo
Halmashauri ya Wilaya ya Uyui zote za Mkoani Tabora na Kata Sindeni Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni, Kata ya Potwe Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Kata ya Kwashemshi
Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na Kata ya Bosha Halmashauri ya Wilaya ya
Mkinga zote za Mkoa wa Tanga.
Kata zingine ni Kata ya Mahege katika
Halmashauri ya Kibiti mkoa wa Pwani, Kata ya Bunamhala katika Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Kata ya Njoro na Kalemawe katika Halmashauri
ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kata ya Mnavira katika Halmashauri ya
Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, Kataya Kinyika katika Halmashauri ya Wilaya ya
mkoa wa Njombe.
Kailima ametaja Kata zingine zitakazo fanya
uchaguzi ni Kata ya Magubike katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani
Morogoro na Kata ya Mbede katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ya mkoa wa
Katavi.
Amesema ratiba ya uchaguzi huo itaanza na
utoaji wa fomu za uchaguzi kwa wagombea kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni , 2023
huku uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hizo ukifanyika Juni 30 mwaka huu.
Kailima amesema vyama vitakavyopata uteuzi
vitaanza kampeni za Uchaguzi tarehe 01 hadi 12 Julai na siku ya kupiga kura
itakuwa tarehe 13 Julai mwaka 2023.
“Tume inatumia nafasi hii kuvikumbusha vyama
vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi uzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi,
Taratibu, Miongozo na maelekezo katika kipindi cha uchaguzi huu mdogo” alisema
Kailima.
Toa Maoni Yako:
0 comments: